TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, January 30, 2012

TIMU YA OLDUVAI KIDS YAIBUKA KIDEDEA KOMBE LA KUHAMASISHA UPIMAJI VVU


Na.Ashura Mohamed -Arusha
Timu ya mpira wa miguu ya Olduvai Kids iliyopo mkoani hapa imeibuka mshindi katika fainali za kombe la kuhamasisha vijana kupima virusi vya ukimwi kwa kuichapa timu ya kaloleni B Magoli 2-0 mechi iliyochezwa jana katika viwanja vya kumbukumbu vya sheikh Amri Abeid mjini arusha.
Akiongea mara baada ya kumalizika kwa mechi hiyo mratibu wa tamasha hilo Samweli Mpenzu amesema kuwa lengo la tamasha hilo ni kuwawezesha vijana kuwa pamoja kupitia michezo pamoja na kutambua afya kwa kuwa michezo ni afya ili kijana anapogundulika kuwa na virusi vya ukumwi basi aweze kufuata ushauri nasaha.
Mpenzu amesema kuwa kupitia tamasha hilo vijana wameweza kuwa pamoja kupitia michezo hiyo pia wamepata fursa nyingine ya kupima virusi vya ukimwi ili kujua afya zao na jinsi ya kujikinga ambapo huduma hiyo pia ilikuwa inapatikana katika viwanja hivyo.
Pia amewashukuru vijana wote waliojitokeza pamoja na timu zote kumi kwa kuwa bila wao tamasha hilo lisingekuwa na ushindani ambapo amesema tamasha hilo pia litafanyika tena mwezi wa pili ambapo safari hii itakuwa ni upande wa wanawake.
Naye mgeni rasmi katika tamasha hilo katibu wa chama cha mpira wa miguu wilaya ya Arusha Zakayo Mjema amesema kuwa tamasha hilo liliandaliwa na YES Tanzania pamoja Tackle Afrika ambapo amewataka wadhamini hao kufanya liwe endelevu.
Mjema amesema kupitia nafasi yake wapo tayari kushirikiana na wadau wa michezo mkoani hapa ili kuwafanya vijana kuwa bise kuliko kukaa bila shughuli maalum ya kufanya pamoja na kuinua soka la mkoa wa Arusha.
Mshindi wa pili katika tamasha hilo ni timu ya Kaloleni B,mshindi wa tatu ni timu ya Intersports na timu zilizoshiriki ni CIDT,Younglife,Caroline Ranges,Arusha Talent, na Young Kids ambapo mshindi wa kwanza aliondoka na kombe na timu zote zilipata hati ya ushiriki.

No comments:

Post a Comment