TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, February 3, 2012

RAUNDI YA 16 LIGI KUU YA VODACOM KUENDELEA KESHO

Mzunguko wa 16 wa Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara unaanza kesho (Februari 4 mwaka huu) kwa mechi tatu. Coastal Union itakuwa mgeni wa Moro United kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam.
Nayo Villa Squad itakuwa mwenyeji wa Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Ruvu Shooting na Polisi Dodoma zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani.
Viingilio kwa mechi ya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam vitakuwa sh. 3,000 kwa viti vya bluu na kijani, sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP B na C, sh. 15,000 kwa VIP A wakati Uwanja wa Chamazi ni sh. 10,000 kwa Jukwaa Kuu na sh. 3,000 mzunguko. Kwa mechi ya Mlandizi kiingilio ni sh. 2,000 kwa mzunguko wakati Jukwaa Kuu itakuwa sh. 5,000.
Pia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefanya mabadiliko ya muda wa kuanza mechi za ligi hiyo kwa kituo cha Dar es Salaam. Mechi zinazochezwa wikiendi kwenye Uwanja wa Taifa zitaaza saa 10 kamili jioni wakati zile zinazochezwa siku za kazi zitaanza saa 10.30 jioni. Mechi zote za Uwanja wa Azam- Chamazi zitaanza saa 10 kamili jioni.

No comments:

Post a Comment