TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, February 1, 2012

MASHUJAA MUSICA YATIMUA BAADHI YA WANAMUZIKI

Aliyekuwa Kiongozi wa Bendi ya Mashujaa Musica-Jado Fidifoce(kulia), akiwa na Meneja wa Bendi hiyo, Khamisi,
Bendi ya Mashujaa Musica ya jijini Dar es Salaam, imetangaza kuwafukuza kazi baadhi ya wanamuziki wake kwa kile walichokiita Utovua wa nidhamu,
akizungmza kwa njia ya Simu Meneja wa Bendi hiyo, Khamisi Khamis, amesema leo kuwa uhamuzi wa kuwaachisha kazi wanamuziki hao umetokana na tabia zao kushindwa kuvumilika katika kundi hilo ambapo wamekuwa wakisababisha upotevu wa amani mara kwa mara.
aidha panga hilo ambalo limepita pia kwa aliyekuwa kiongozi wa kundi hilo, Jado Fid Foce, ambaye hivi karibuni alijiengua katika nafasi yake ya Uongozi kwa madai ya kupisha kiti hicho kukaliwa na Mtu mwingine, 
wengine waliokumbwa na Pangua pangua hiyo ni pamoja na Pasia Budansi(Mwimbaji),Dulla Ngoma(Mpiga tumba), Jimmy Adoly(mwimbaji), Zidane Chapati(Rapa), wakati kwa upande wa wacheza shoo walioachishwa kazi ni Kevini, Mwiba, Baby White, jack pamoja na Kamodee.
Mashujaa Musica Bendi hivi sasa inakuja kwa kasi katika ulimwengu wa burudani ya miziki ya dansi kiasi cha kuziogopesha baadhi ya bendi kongwe zikiwemo za Twanga, FM Academia, Extra Bongo, Mapacha watatu na zingine nyingi, 
siku ya leo jumatano bendi hiyo inapatikana katika Ukumbi wake wa nyumbani wa Mashujaa na siku ya ijumaa bendi hiyo inakuwa katika ukumbi wa Business Complex  Victoria barabara ya kuelekea Mwenge.

No comments:

Post a Comment