TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, January 30, 2012

Wakulima zao la Karafuu Kisiwani Pemba watakiwa kutohifadhi Karafuu zao Majumbani

Na:- Marzuku Khamis Maelezo Pemba.
Wakulima wa zao la Karafuu Kisiwani Pemba wametakiwa kutohifadhi Karafuu zao Majumbani na badala yake waziopeleke katika vituo vya ununuzi vya Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar (ZSTC) kwa ajili ya kuziuza badala ya kuzirundikiza Majumbani mwao kama inavyojitokeza hivi sasa
Wamesema kufanya hivyo kutawaepushia na vitendo vya Wizi na pia kuweza kupata uzito mkubwa wa Karafuu zao zitakazowapatia pato zuri zaidi
Wakuu wa vituo mbali mbali vya ZSTC vya unuzi wa karafuu waliyasema hayo wakati walipotembelewa na kamati ya kitaifa yakudhibiti zao la Karafuu Zanzibar wakati walikpokuwa wakitembelea vituo mbali mbali vya ununuzi wa karafuu pamoja na vikosi vya ulinzi wa zao hilo kisiwami Pemba.
Wamesema kuwa ukweli hivi sasa Msimu wa Uchumaji wa Karafuu upo ukingoni lakini kilichobainika kuwa bado Karafuu zimo Katika majumba mbali mbali ya wakulima hivyo ni wajibu wa kila mkulima hivi hivi sasa kuzipeleka kwenye vituo vya ZSTC kwa kuziuza jambo ambalo litakuwa ni faida kubwa kwao na serikali kwa jumla.
Wakizungumzia juu ya suala la malipo ya Wakulima wanaouza karafuu zao humo vituoni wamesema kuwa hakuna hata Mkulima mmoja aneidai ZSTC na mtu yoyote anaekwenda kuuza Karafuu zake mara tu baada yakuuza anapewa malipo yake yote.
Aidha wakuu hao wa vituo wamesema kuwa kwa ujumla kazi ya ununuzi wa Karafuu imekwenda vizuri na mashirikiano kutoka kwa wauza karafuu pia yalikuwa mazuri na makubwa na kutowa wito kwa Wakulima kuharakisha kuzipeleka Karafuu zao Kuziuza hivi sasa Katika vituo vya ZSTC kwani wasije kupata usumbufu pale ZSTC itakapoamuwa kupunguza vituo hivyo Vijijini na kuvibakisha vituo vya Mijini.
Mkuu wa Mkoa Kusini Unguja Mustafa Mohamed Ibrahim ambae ni mjumbe wa kamati ya kitaifa ya kudhibiti zao la karafuu Zanzibar amesema kuwa amefarajika sana na kazi nzuri inayoendelea kufanyika katika utekelezaji wa kazi za ununuzi wa Karafuu na kuwataka Wakuu hao kuendelea kutoa Mashirikiano kwa Wakulima wa zao la Karafuu kwa kuwakumbusha kuzipeleka kuuza karafuu zao haraka kwenye vituo hivyo vya ZSTC na kutozihifadhi majumbani.
Katika ziara hiyo wajumbe wa kamati ya kudhibiti zao la Karafuu Zanzibar ambayo ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa Kusini UngujaMustafa Mohamed Ibrahim ilitembelea Ghala kuu la kuhifadhia karafuu lilioko Mkoani, Kituo cha ununuzi wa Karafuu cha Kiwani,Chanjaani,Bwagamoyo, Raha,Mgogoni,Kisiwani, Mtambile na Chumbageni Wambaa.
Pia Wajumbe wa kamati hiyo walitembelea kambi za Vikosi vya Kudhibiti Magendo vya Chaanjaani na Mkuumbuu.

No comments:

Post a Comment