TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, January 8, 2015

Vijana wa Mkoa wa Kilimanjaro wapigwa msasa kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.

unnamed1Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa kulia akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Bw. Jamhuri David Willium walipomtembelea ofisi kwake wakati wa ziara ya Uhamasishaji kwa Vijana kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana leo Mkoani Kilimanjaro Wilaya ya Mwanga.
unnamed2Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Bw. Shaibu Ndemanga akizungumza na wajumbe kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo walipomtembelea ofisini kwake kabla ya kwenda kuongea na vijana kutoka Wilaya za Mwanga, Same na Moshi vijijini kuwahamasisha na kutoa elimu kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana leo Mkoani Kilimanjaro Wilaya ya Mwanga.
unnamed3Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa akitoa elimu kwa Vijana wa Mwanga, Same, na Moshi Vijijini kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana wakati wa uhamasishaji wa Mfuko huo leo Mkoani Kilimanjaro Wilaya ya Mwanga.
Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Amina Sanga akitoa elimu kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kwa Vijana wa Wilaya za Mwanga, Same na Moshi Vijijini leo Mkoani Kilimanjaro. Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo
………………………………………………………….
Na: Genofeva Matemu – Maelezo Vijana wametakiwa kujitambua na kuwa na fikra yakinifu na bunifu ili kuweza kutatua matatizo yanayowalenga na kuweza kuwa na maamuzi katika shughuli wanazozifanya. Hayo yamesemwa leo na Mwamasishaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Ester Riwa wakati wa semina ya Vijana kuhusu uhamasishaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana leo Mkoani Kilimanjaro katika wilaya ya Mwanga. Bibi. Riwa amewashauri vijana kutumia changamoto ya ukosefu wa ajira kuwa fursa ya vijana kujishughulisha kwa kujiunga katika vikundi, kusajiri vikundi hivyo na kuandika andiko la Mradi litakaowawezesha kupata mkopo unaotolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ili waweze kuachana na tabia ya kukaa vijiweni na kuweza kuendeleza jamii inayowazunguka. “Vijana mnapaswa kutimiza wajibu wenu kwa kujishughulisha na kuachana na zana potofu yakukaa mitaani mkisubiri kufanyiwa maendeleo na serikali ni vyema mkajiunga katika vikundi imara na kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kujenga taifa letu kwani vijana ni taifa la leo” amesema Bibi Riwa. Akizungumza wakati wa semina hiyo Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele amewataka vijana kutokuwa na dhana potofu ya Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kuwa umewaletea fedha nyingi hivyo kuibua miradi mingi isiyokua halisi kwani lengo la mfuko huo ni kuwasaidia vijana kuwa na umoja katika kusimamia na kutumia fedha hizo kwa makini ili waweze kufikia malengo waliyoyakusudia. Aidha Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Bw. Shaibu Ndemanga ameishukuru Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuutuma ujumbe uliofika Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga kutoa elimu ya uhamasishaji kwa vijana kwani vijana wa Mwanga wanahitaji sana elimu hiyo na wao kama viongozi wa Wilaya wanajitahidi kuwaelimisha vijana na kuwasaidia pale wanapohitaji msaada kutoka kwao. Akichangia wakati wa semina hiyo Bw. Musa Michumvu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga amewapongeza wahamasishaji kutoa Wizara ya Habari na kuomba elimu hiyo kwa vijana kuendelea kutolewa mara kwa mara kwani vijana wanahitaji kuelimishwa ili waweze kuthubutu na kujitegemea kwa maendeleo ya jamii na taifa.

No comments:

Post a Comment