Fainali
 ya Michuano ya Michezo kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, 
imeshereheshwa na burudani kabambe kutoka kwa wasanii mbali mbali wa 
muziki, lakini pia burudani kubwa ilikuwa ni kwa wanafunzi walioonyesha 
vipaji vyao kutokana na kuwa na khari wakti wote wa kujieleza, kujibu 
maswali ambapo wanafunzi mbali mbali wameweza kujipatia zawadi kutoka 
Kampuni ya Simu za Mkononi Airtel Tanzania, ambao ndiyo Wadhamini Wakuu 
walioweza kufanikisha Shughuli hiyo, ambayo kwa Wanafunzi hao pia 
ilikuwa ni kupata Timu za College zitakazoshiriki Ligi ya Dar es Salaam 
inayoshirikisha pia Vyuo vya Pwani na Bagamoyo, Michuano ya Kutafuta 
Timu za Vyuo ni Mpango unaoratibiwa na Kampuni ya Miss Demokrasia 
Tanzania, iliyopewa dhima na wenye haki Miliki ya kuwa waamdaji wa 
Michezo hiyo Kila Mwaka.
Vyuo
 ambavyo Tayari vimefanikiwa kuingia kwenye kinyang'anyiro hicho cha 
NACTE INTER COLLEGE  Championship Mpaka sasa baada ya kushinda Michezo 
yake kwenye Makundi kwa njia ya Mtoano, iliyofanyika kwenye viwanja 
mbali mbali vya  vyuo ikiwemo D.I.T, Shirika la Elimu Kibaha, Ustawi wa 
Jamiii, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), Viwanja vya Mabibo Hosteli, 
N.I.T na Bandari College, Wenyeji wameweza kuingia hatua ya pili pamoja 
na timu za I.F.M, CBE, TRA,MUHIMBILI, COET,COSS,UDBS.
Wengine ni Mwalimu Nyerere Memorial Academy,Institute of Adult Education, Kilimanjaro Institute College, St. Joseph 
College, Zoom Polytechnic College , Tanzania Institute of Accountancy (TIA,Njuweni Institute of Hotel, Catering &
Tourism Management, Bagamoyo College of Arts (TaSUBa), St. Mary Teachers College, na  Dar es salaam City College (DACICO).
 Zaidi
 ya Vyuo mia nne 400 vilivyopata usjali wa NACTE Tanzania vilitakiwa 
kushiriki michezo hiyo lakini kutokana na sababu mbali zilizowasilishwa 
na vyuo baadhi yao hawataweza kushiki kwa mwaka huu kutokana na kile 
walichosema Maandalizi ya kustukiza ambapo  wamewataka waandaaji kutoa 
taarifa mapema ili kila chuo kiweze kuwaandaa wachezaji kwa ajili ya 
kushiriki huku vyuo vingine vikiwa havina wachezaji wa kuweza kushiriki.
 Ratiba
 ya Michuano hiyo inaanza April ambapo timu hizo zitacheza ligi ya 
Nyumbani na Ugenini na itachuku siku 45 hadi kumalizika zikiwa ni siku 
za wikiend kuanzia April mosi hadi Mey 24, sambamba na Vyuo vya Mikoa ya
 Kanda ya Ziwa, kanda ya Kaskazini, kanda ya  Kati, Kanda ya Kusini, na 
Kanda ya Zanzibar zitashiriki Michuano hiyo na timu zitakazofanikiwa 
kuibuka na Ubingwa kwa kila kanda zitakutana kutafuta Bingwa wa chuo bora katika michezo Tanzania(NACTE) (The best in sports college Tanzania).
(Picha na Mpiga Picha wa MIDETA Entertainment)
No comments:
Post a Comment