Mtaalam
 wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce 
Temu akimtambulisha Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na 
mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, 
Alvaro Rodriguez (katikati) alipoitishia mkutano na waandishi wa habari 
jijini Mwanza mara baada kuhitimisha ziara zake Kanda ya ziwa. Kushoto 
ni Mshauri wa masuala ya haki za binadamu kutoka ofisi ya mratibu mkazi 
wa UN Tanzania, Bi. Chitralekha Massey.
Na Mwandishi wetu, Mwanza
MRATIBU
 wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika 
la maendeleo la Umoja huo, UNDP, Alvaro Rodriguez ameutaka uongozi mkoa 
wa Mara kuanzia Polisi hadi serikali ya mkoa kuweka kipaumbele kumtafuta
 binti albino ambaye ametekwa na watu wasiojulikana siku 14 zilizopita.
Hayo aliyasema jana kwenye mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika jijini Mwanza
 baada ya kutembelea mkoa ya kanda ya ziwa ikiwemo Mara, Shinyanga na 
Mwanza kuangalia miradi inayotekelezwa na Umoja wa Mataifa pamoja na 
masuala ya haki za binadamu.
Alisema
 serikali kupitia Mkuu wa mkoa na Kamanda wa polisi mkoa wahakikishe 
wanaendelea kumtafuta na kulipa suala la Pendo Emmanuel (4) kipaumbele .
Pendo
 alitekwa na watu wasiojulikana baada ya mlango wa nyumba yao kuvunjwa 
Desemba 27,2014 kwa jiwe la fatuma katika kijiji cha Ndami tarafa ya 
Mwamashinda,wilayani Kwimba mkoani hapa ambapo hadi sasa bado 
hajapatikana.
Aidha
 aliwataka wananchi na viongozi kuhakikisha usalama wa watu wenye 
ulemavu kwani wao ni binadamu kama binadamu wengine na wanahitaji haki 
yao ya msingi ya kuishi bila hofu na manyanyaso kutoka kwa jamii 
inayowazunguka.
Mwakilishi
 huyo wa Umoja wa mataifa alisema katika mkutano huo kwamba hata 
kurundikana kwa watoto walemavu wa ngozi katika kituo cha Buhangija 
kilichopo Shinyanga ni matokeo ya mauaji yanayoendeshwa dhidi yao na 
kusema suluhisho la tatizo hilo ni jamii kuwakubali watu wenye ulemavu 
wa ngozi.
Tayari
 watu 15 wanashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi wa kuhusika na 
uporwaji wa mtoto huyo akiwemo baba mzazi, Emmanuel Shilinde.
Pamoja
 na kuzungumza na waandishi wa habari mkoani Mwanza, kuelezea ziara yake
 katika Ukanda wa Ziwa, Mwakilishi huyo pia alizuru wilaya ya Magu na 
kukagua mradi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto 
,UNICEF, wenye lengo la kuhakikisha haki inatetendeka dhidi ya wale 
wanaonyanyasa watoto na haki zao za kibinadamu zinahesmiwa.
Mratibu
 Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la 
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez 
akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza.
Akiwa
 Magu alifurahishwa na mashikamano unaoneshwa na serikali na wadau 
wengine kuhakikisha kwamba mradi huo unafanikiwa hasa katika kuwezesha 
watu kutambua haki za msingi za watoto na kutoa msaada wa kisaikolojia 
kwa watoto waliofanyiwa unyanyasaji na kuanzishwa kwa dawati la watoto 
na jinsia vituo vya polisi.
Hata hivyo aliambiwa changamoto zinazoambatana na ukusanyaji wa taarifa hasa katika maeneo ya ndani zaidi.
Katika
 mazungumzo yake na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magese Mulongo, Umoja wa 
Mataifa na Serikali ya Mkoa walikubaliana kwamba usalama wa wananchi 
hasa watoto nay ale makundi maalumu ndio suala la msingi ambalo pande 
zote hizo mbili itatilia maanani.
Akiwa
 Shinyanga, Mwakilishi huyo Alvaro Rodriguez nalea kituo cha kulelea 
watoto wenye ulemavu wa ngozi , wasiiona na viziwi Buhangija na kujionea
 hali halisi ya mrundikano wa watoto.
Kituo hicho kina watoto 220 wenye ulemavu wa ngzoi ambao walikimbiziwa hapo baada ya usalama wao kuwa shakani.
Alifurahishwa
 na juhudi zinazofanywa na wadau mbalimbali kuimarisha hali ya ustawi 
katika kituo hicho ambacho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali 
zikiwemo za mrundikano wa watoto, afya na lishe.
Mkutano
 na waandishi wa habari uliotishwa na Mratibu Mkazi wa mashirika ya 
Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa 
Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez ukiendelea.
Alisema
 akiwa hapo kwamba kama sehemu ya ajenda ya Umoja wa mataifa kusaidia 
kulinda haki za binadamu na kuhakikisha wale wanaoishi na ulemavu wa 
ngozi wanaendelea kustawi na haki zao zinaoheshimiwa, mwakilishi huyo 
alisema Umoja wa Mataifa utaendelea kutoa msaada kwa kundi hilo.
 Pia 
alifanya mazungumzo na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na mkuu wa wilaya
 hiyo Anna Rose ambapo walikubaliana kwamba suluhu ya mwisho ni kwa 
watanzania kuwakubali wenye albinizim kama wenzao na kuacha kuwatafuta 
kuwaua kwa imani za kishirikina.
Akiwa
 mkoani Mara alishiriki katika hafla ya kutunuku vyeti wasichana na 
wavulana waliofuzu mafunzo ya miezi miwili yenye lengo la kuwaingiza 
katika jamii bila kukutwa au kufanyiwa tohara yenye maumivu (kwa 
wavulana).
Mafunzo
 hayo ni mchango wa Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la UNFPA wenye
 lengo la kukabiliana na mila potofu ikiwamo ya ukeketaji na mimba za 
utotoni zinazotokana na mabinti kuolewa wakiwa wadogo.
Katika
 mazungumzo na mkuu wa mkoa wa Mara, kapteni mstaafu Asery Msangi, Umoja
 huo ulikubaliana na serikali ya mkoa kuendelea kushirikiana katika 
kuhakikisha haki za msingi za binadamu zinaheshimika na wananchi 
kuelimishwa kuhusu haki hizo.
No comments:
Post a Comment