Wananchi na viongozi wa manispaa ya Iringa watakiwa kujitolea katika
 maswala mbalimbali yahusuyo jamii kwa kuwajibika ipasavyo hasa katika
 swala la kufanya usafi katika mazingira yanayotuzunguka.
 Akizungumza na nuru fm  mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM taifa FRANK
 KIBIKI amesema kuwa ameamua kufanya usafi katika maeno mbalimbali ya manispaa ya iringa kwa kuwa kikundi chao kimejitolea kufanya kazi hiyon
 pamoja na kujitambulisha kwa uongozi wa halmashauri ya manispaa.
 KIBIKI ameongeza kuwa kiongozi lazima uwe mfano kwa jamii husika katika kuleta maendeleo mbalimbali hasa kuwajengea vijana uwezo wa kujitambua na kupenda kujifunza na kuijijali wao wenyewe hasa swala la usafi.
 KIBIKI ameongeza kwa kusema kuwa kila mtu anayeishi duniani anaweza
 kuzibzdili changamoto kuwa fursa ambazo zitakuwa na faida kubwa kwa
 jamii husika lakini akasema kuwa sio kiasi gani cha fedha
 alizizoziacha dunia buli ni familia gani ya familia aliyoiacha
 duniani.
 Aidha KIBIKI amewata wananchi wa manispaa  kuwafundisha vijina jinsi
 gani ya kufanya usafi hivyo watakuwa wamechangia kuioka jamii katika
 swala afya kwa kuwa wananchi wote watakuwa wanajua umuhimu wa wa
 kutunza mazingira.
 KIBIKI amemalizia kwa kuwataka wananchi kuwa wasafi na kuwaridhisha
 vijana kujua na kujifunza juu ya kufanya usafi hivyo usafi ukianzia
 nyumbani  basi hata mitaa yetu itakuwa misafi na tutakuwa
 tumewatengezeza viongozi wazuri.
No comments:
Post a Comment