Waziri
 wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Haji Omar
 Kheri akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Tagi mpya ya Shirika la 
Bandari Zanzibar ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za kutimiza miaka 
51 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar. 
Waziri
 wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Haji Omar
 Kheri akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Tagi mpya ya Shirika la 
Bandari Zanzibar ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za kutimiza miaka 
51 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar. 
Tagi
 iliyozinduliwa ikirusha maji ikiwa ni majaribio ya kuzima moto iwapo 
tatizo hilo litajitokeza. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
……………………………………………………………………………
Na Miza Kona Na Abdalla Ali – Maelezo Zanzibar
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, 
Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Haji Omar Kheri amewataka 
wafanyakazi wa Shirika la Bandari Zanzibar kufanya kazi kwa juhudi na 
ufanisi kwa lengo la kuleta maendeleo na mabadiliko nchini.
Hayo ameyaeleza huko katika 
Shirika la Bandari Zanzibar wakati akizindua Tagi mpya ya Shirika hilo 
MV Shuwari ikiwa ni miongoni mwa  shamrashamra za kusherehekea miaka 51 
ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema bandari ni chachu ya 
maendeleo katika nchi yoyote Duniani na muhimili mkuu wa kuleta 
maendeleo na mabadiliko yatakayofanywa kwa ufanisi na juhudi kubwa 
zitakazoweza kuinua uchumi wa  nchi.
Amefahamisha kuwa utendaji wa kazi
 unategemea rasilimali watu na vifaa vya kisasa vinavyo kwenda sambamba 
na mazingira ya kazi yatakayoleta maendeleo na mabadiliko ya haraka 
katika kutoa huduma za utendaji.
“Utendaji wa kazi unategemea 
rasilimali watu na vifaa vya kutosha na vya kisasa ambavyo vinakwenda 
sambamba na mazingira ya kazi ambavyo vitaleta maendeleo na mabadiliko 
ya haraka katika kutoa huduma za utendaji”, Alieleza Waziri Omar.
Aidha Waziri Omar ameeleza kuwa 
ufinyu wa nafasi ya kuhifadhia mizigo bandarini hapo, pamoja na 
Wafanyabiashara kutoondosha Makontena yao kwa wakati ndio changamoto 
kubwa zinazoikabili bandari hiyo.
Waziri Omar pia amewataka 
wafanyabiashara kuchukua juhudi za kutoa mizigo yao bandarini kwa wakati
 ili kuondosha msongamano uliopo na kulipa ushuru wa mizigo hiyo ili 
kuliongezea pato la Taifa.
Amesema madhumuni ya Tag hiyo ni 
kuimarisha ufungaji na ufunguaji wa meli bandarini hapo hivyo mategemeo 
makubwa ni kuona kuwa inatumika ipasavyo kwa kufuata ushauri na 
maelekezo ya wataalamu kwa lengo la kuleta maendeleo ya bandari na taifa
 kwa ujumla.
Nae Mkurugenzi mkuu wa Shirika la 
Bandari Zanzibar Cpt. Abdalla Juma Abdalla amesema Tagi Mv Shuwari 
tayari imeshaanza kazi ya kusaidia kufunga na kufungua meli gatini 
ambayo inauwezo wa kukabiliana na  majanga ya moto pamoja kusaidia 
kuokoa maisha ya watu inapotokea ajali ya meli au boti baharini.
Amesema Tagi hiyo imejengwa kwa 
udhamini wa kampuni ya Damen Shipyards ya Uholanzi kwa kushirikiana na 
Shirika la Bandari la Zanzibar na imegharimu Tsh.zaidi Bilioni 10 ambapo
 Bilioni 6.9 ni mkopo kutoka Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) na ghrama 
zilizobaki zimelipwa na Shirika la Bandari.
Tag hiyo ina urefu wa mita 22.64, 
upana mita 7.84, kina cha kueleya mita 3.50, nguvu zake 2720 HP, mwendo 
11.70 knots, nguvu za kuvuta tani 38, na uzito wa tani 140 inatarajia 
kuleta maendeleo makubwa bandarini hapo.
No comments:
Post a Comment