Makamu
 wa Pili wa  Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema lengo  la 
kuandaa  Tamasha la Biashara Zanzibar ni kushajihisha ukuwaji wa Uchumi 
 na kuirejeshea Zanzibar hadhi yake ya zamani  ya kuwa kituo kikuu cha 
Biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Amefahamisha kuwa Tamasha hilo 
ambalo litawakutanisha Wafanya Biashara wakubwa kutoka Zanzibar na 
sehemu nyengine  litatoa fursa  kwa wafanya biashara wadogo  na wanunuzi
 wengine wa kawaida kupata bidhaa muhimu kwa bei ya kawaida.
Hayo aliyasema wakati wa ufunguzi 
wa Tamasha la Pili la  Biashara la mwaka 2015 huko katika Viwanja vya 
Maisara Mjini Zanzibar ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za kutimiza  
miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
“Wafanya Biashara na Wajasiria 
Mali waitumie fursa hii adhimu ipasavyo kwa lengo la kuendeleza Biashara
 hapa Zanzibar na kupata huduma muhimu”Alisema Balozi Seif.
Balozi Seif alifahamisha kuwa 
Matamasha ya Biashara  hutoa   fursa ya kukuza Sekta ya Utalii  kwa 
  kuhudhuriwa na wageni mbali mbali kutoka nje.
Alisema  nchi nyingi Duniani 
zinafaidika na Matamasha makubwa ya kibiashara kama vile Tamasha la 
Dubai Shoping  Festival linalokusanya zaidi ya Wageni Milioni 4.4 na 
kuchangia pato la Taifa zaidi ya Bilioni 15.
Alieleza kuwa Serikali  itaendelea
 kushirikiana na Wafanya Biashara wa Zanziba,r Tanzania na Afrika 
 Mashariki katika kuhakikisha sekta ya Biashara inazidi kukua na 
kuimarika  ili kuongeza pato la Taifa .
Sambamba na hayo alisema Serikli 
itaendelea kushughulikia  changamoto zinazoikabili Sekta ya Biashara 
kama vile upatikanaji wa vifungashio, kuanzisha mfumo  wa nambari za 
utambulisho wa bidhaa (barcodes) na  kufikia Viwango vya Biashara 
Kimataifa.
“Ni vyema Matamasha ya  aina hii 
yakajumuisha maonyesho ya Utamaduni wa Mzanzibari zikiwemo kazi za 
Sanaa, Vyakula vya asili na Muziki wa mwambao ambao unaendelea 
 kutoweka” Alisema Makamu wa Pili.
Ameitaka Wizara ya Biashara, 
Viwanda na Masoko kulitangaza zaidi Tamasha la Biashara na kuanzisha 
eneo maalum la maonyesho ya Biashara  hapa Zanzibar.
Balozi Seif alitoa shukurani zake 
kwa Taasisi za Serikali na  watu binafsi, Makampuni, Wafanya Biashara  
wa ndani na nje ya nchi kwa  kushiriki  Tamasha hilo.
Nae Waziri wa Biashara Viwanda na 
Masoko  Nassor Ahmed Mazurui  alisema  zaidi ya Wafanya Biashara  160 
watashiriki Tamasha la mwaka huu.
Alisema Tamasha hilo linalengo la 
kuitangaza Zanzibar Kiutalii na Kibiashara kwa kuandaa  mazingira mazuri
  ili kuleta kivutio kikubwa kwa  washiriki na wanunuzi.  
No comments:
Post a Comment