Mbunge
 wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh aziz Abood Akijibu Hoja Mbalimbali Kuhusu
 kero Zinazowakabili wakazi wa Kata ya Bigwa Katika Ziara yake ya 
Kutembelea Kata Mbalimbali za Jimbo la Morogoro Mjini.Mh Abood Aliata 
nafasi ya Kuongea na wakazi wa Mitaa wa Mitaa Mbalimbali inayounda Kata 
ya Bigwa.Mh Abood alijibu na Kutatua Kero Mbalimbali zinazowakabili 
wakazi wa Kata Hiyo.Mbunge Huyo alitoa Majibu Kuhusu Kero ya Umeme,Maji ,Barabara na Nyinginezo.Pia Mh Abood alitoa Misaada Mbalimbali iliyogarimu zaidi ya Milioni 20 Katika Kata ya Bigwa.
Mbunge
 wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh aziz Abood akiwa kwenye banda la Mama 
Lishe maarufu Kama Mama Ntilie Ili Kujionea na kujua  Changamoto 
Zinazowakabili wamama hao katika kazi yao Hiyo wakati wa Ziara yake ya 
Kutembelea Kata ya Bigwa Jimbo la Morogoro Mjini
Baadhi ya Misaada aliyotoa Mbunge huyo kwa Wakazi wa Kata ya Bigwa.
Mbunge
 wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Akikabidhi vifaa Mbalimbali 
kwa Vikundi vya wakina Mama wanaojihusisha na Shuguli za Mama Lishe 
Katika Mitaa ya Vituli, Bomela, Korogozo,Mungi, na Mgolole Iliyopo Kata 
ya Bigwa.
Wakazi wa Kata ya Bigwa wakiwa wamemzunguka Mbunge wao
Mbunge
 wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akisikiliza Kwa Makini Kero 
iliyokuwa Ikiwasilishwa na Mmoja wa wakazi wa Mtaa wa Mgolole kata ya 
Bigwa alipotembelea Mtaa huo kusikiliza na Kutatua Kero za Wakazi wa 
Mtaa Huo.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood akiongea kwa Msisitizo kuhusu watendaji kushugulikia Kero la wananchi wa Kata ya
Bigwa kwa haraka.
Badhi ya Wakina Mama wanaojishugulisha na kazi ya Mama Lishe wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood
Mbunge
 wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Akiwa Amezungukwa na Vijana 
wa Kata ya Bigwa wakimweleza Kuhusu kero ya Ajira Na Michezo Ambapo 
Mbunge Huyo alijibu Hoka Hizo kwa Kuwakabidhi Mpira wa Miguu .Kuhusu 
Ajira Mh Abood aliwaagiza Vijana Hao Kujiunga kwenye Vikundi vya Kufanya
 Shuguli za Maendeleo na yeye atawawezesha kwa Kuwapa Mitaji.
Mbunge
 wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akiwa Nyumbani kwa Balozi wa 
CCM Mtaa wa Misongeni B Kata ya Bigwa Ndugu Omary Iddy aliyemgonjwa 
alipofika Kumjulia hali.
Mbunge
 wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh aziz Abood Akiwa Nyumbani kwa Balozi wa 
CCM Mtaa wa Misongeni B Iliyopo Kata ya Bigwa Manispaa ya Morogoro Ndugu
 Omary Iddy aliyemgonjwa kwa Muda Mrefu Alipofika Kumpa Pole.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh aziz Abood Aliofika Kuhani Msiba wa Bi Nuru Binti Ally Ngozi wa Kata ya Bigwa. 



No comments:
Post a Comment