Katibu
 Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi 
mbalimbali waliohudhuria kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika 
kwenye uwanja wa Tangamano mjini Tanga, katika mkutano huo Kinana 
ametumia muda mwingi kuwashukuru wananchi wa mkoa wa Tanga na watanzania
 kwa ujumla kwa kukiamini chama cha Mapinduzi na kukipa ushindi wa 
kishindo katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Disemba 14 
mwaka jana ambapo Chama cha Mapinduzi mkoa wa Tanga kimeshinda kwa 
asilimia 97% mkoa huo ukishika nafasi ya pili huku mkoa wa Iringa 
ukiongoza kwa ushindi wa asilimia 98%. ambapo ushindi wa jumla kwa nchi 
nzima CCM kimeshinda kwa asilimia 81%, Katika mkutano huo pia Kinana 
amewaasa wana CCM kutotafuta mchawi  nje ya ila mchawi ni CCM wana CCM  
wenyewe na akaongeza kwamba katika kujiandaa na uchaguzi mkuu ujao 
kigenzo muhimu kitakachoangaliwa sana ni uadilifu wa viongozi. 
Katibu
 Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika 
mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Tangamano mjini Tanga. 
Umati Mkubwa uliohudhuria kwenye mkutano huo 
Kutoka
 kushoto ni mwanamuziki Mzee Yusuf kiongozi wa bendi ya Taarab ya Jahazi
 na Mbunge wa jimbo la Korogwe vijijini Profesa Maji Marefu wakifuatilia
 mkutano huo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo katika mkutano huo.
Mwanamuziki
 Mzee Yusuf kiongozi wa bendi ya Taarab ya Jahazi akiwasalimia wananchi 
na mashabiki wake wakati wa mkutano huo wa hadhara.
Katibu
 Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza  jambo na baadhi ya 
viongozi katika meza kuu kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Handeni Mh.Muhingo
 Rweyemamu
Mwanamuziki Mzee Yusuf kiongozi wa bendi ya Taarab na wanenguaji wake wakifanya vitu vyao jukwaani.
mwanamuziki Mzee Yusuf kiongozi wa bendi ya Taarab na wanenguaji wake wakifanya vitu vyao jukwaani.
Mh. 
Januari Makamba Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia akimpongeza 
mwanamuziki Mzee Yusuf mara baada ya kutumbuiza katika mkutano wa 
hadhara wa Chama cha Mapinduzi uliofanyika kwenye viwanja vya Tangamano 
mjini Tanga.
Nyoomi ya kutosha
Aliyekuwa
 mgombea ubunge kupitia chama cha  CHADEMA Tanga mjini Bw. Hassan Omary 
Mbarak akitangaza rasmi kujiunga na CCM mara baada ya kupokea dozi ya 
kutosha kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu. Abdulrahman Kinana 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu. Abdulrahman Kinana akimpongeza Bw.Bw. Hassan Omary Mbarak kwa uamuzi wake wa kujiunga na CCM.
Katibu
 Mkuu wa CCM Ndugu. Abdulrahman Kinana akiagana na wananchi mara baada 
ya kuhutubia mkutano huo wa hadhara kwenye viwanja vya Tangamano mjini 
Tanga.
Wengine walipanda juu ya magari kama wanavyoonekana
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga Ndugu Henry Shekifu akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM ili kuongea na wananchi katika mkutano huo.
Baadhi ya mawaziri na viongozi mbalimbali wakiwa katika mkutano huo













No comments:
Post a Comment