TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, January 7, 2015

Uvamizi ufaransa, 12 wauawa

Watu waliokuwa wamejihami wameshambulia ofisi ya jarida la vibonzo nchini Ufaransa Charlie Hebdo na kuwaua watu 12 huku wengine 7 wakijeruhiwa katika shambulizi linalodhaniwa kuwa la kigaidi
Wanaume wawili waliokuwa wamefunika nyuso zao waliwafyatulia risasi wahariri wa jarida hilo lakini walikabiliwa na polisi ambao pia walifyatuliana risasi nao. 
 Wawili kati ya waliouawa ni maafisa wa polisi huku wengine waliojeruhiwa wakisemekana kuwa hali mahututi
 Msako mkubwa unafanywa na polisi kuwasaka waliohusika na uvamizi huo. Idadi ya wavamizi mwanzo ilisemekana kuwa watu wawili tu lakini wizara ya ulinzi inasema inawasaka wavamizi watatu
 Rais Francois Hollande alisema hapana shaka kwamba waliofanya uvamizi huo waliokuwa magaidi. 
 Wachoraji wanne wa jarida hilo wanaosifika sana akiwemo mhariri mkuu Stephane Charbonnier waliuawa 
Bwana Charbonnier aliyekuwa na umri wa miaka 47 aliwahi kupokea vitisho vya mauaji na tangu hapo amekuwa chini ya ulinzi wa polisi

Hawa ni wachoraji wengine waliouawa katika uvamizi uliofanyika ashubuhi wakati wa mkutano wa kila siku wa wahariri wa jarida hilo 
Baadhi ya waliojeruhiwa wanasemekana kua hali mahututi
Jarida hilo ambao hutolewa kila wiki, limejikuta pabaya hasa baada ya kuwahi kumfanyia istihizai mtume Mohammad wa dini ya kiisilamu picha ambazo ziliwakera sana waisilamu
Vyombo vya habari nchini Ufaransa vimetahadharishwa na kutakiwa kuwa makini na maswala ya usalama hasa baada ya tahadhari kutolewa kwamba nchi hio huenda ikashambuliwa na wapiganaji wa kiisilamu baada ya matukio kadhaa ya kiusalama kabla ya krismasi

No comments:

Post a Comment