Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa 
Tanzania (JWTZ), linatoa taarifa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa 
Tanzania na Amri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete atazindua 
nyumba mpya za makazi ya Wanajeshi eneo la Gongolamboto mnamo tarehe 10 
Januari, 2015,    Saa 3:00 Asubuhi.
Aidha, uzinduzi wa nyumba hizo 
ni sehemu ya nyumba elfu kumi za  mwanzo za makazi ya Maafisa na Askari 
wa JWTZ zilizojengwa katika mikoa mbalimbali hapa nchini kwa lengo la 
kuondoa tatizo la nyumba za makazi kwa Wanajeshi.
Ujenzi wa nyumba hizo za kisasa umefanywa na Kampuni iitwayo ‘Shanghai Construction Group’ ya Jamhuri ya watu wa China.
Waandishi wa Habari wanaombwa kuhudhuria na kufanya ‘Coverage’ katika tukio hili muhimu.
  Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga

No comments:
Post a Comment