Mbunge wa Jimbo la Chalinze, 
Ridhiwani Kikwete (kulia), akipata maelezo kutoka kwa Msimamizi wa 
ujenzi kutoka Kambi ya Mzinga ya JWTZ, Aloyce Mayunga (kushoto) 
alipokwenda kukagua ujenzi wa maabara ya Shule ya Sekondari ya Kiwangwa 
wakati wa ziara ya kikazi ya katika Kata ya Kiwangwa, wilayani Chalinze,
 Pwani leo.Aliwataka wajenzi hao kujenga maabara hayo kwa kuzingatia 
viwango. Katikati ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya 
Bagamoyo, Saleh Mpimbwi.
 Ridhiwani Kikwete akizungumza na 
wakandarasi kutoka Kambi ya Mzinga ya JWTZ wanaojenga maabara ya Shule 
ya Sekondari ya Kiwangwa wakati wa ziara ya kuagua miradi ya maendeleo 
na kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa mbunge miezi sita iliyopita. 
 Ridhiwani akinyoosha juu kadi ya 
Chadema aliyokabidhiwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa  Chadema Kijiji cha 
Masugulu ambaye amehamia CCM katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha
 Mwitemo Kata ya Kiwangwa leo
 Ridhiwani akihutubia wananchi  katika Kijiji cha Mwitemo
 Sehemu ya akina mama wakisikiliza
 kwa makini wakati Ridhiwani Kikwete akihutubia katika Kitongoji cha 
Magogoni, Kijiji cha Msinune, Kata ya Kiwangwa.
 Ridhiwani Kikwete akihutubia wananchi katika Kijiji cha Msinune, Kata ya Kiwangwa.
 Msanii kiongozi wa Kikundi cha 
sanaa cha Chanzala akifanya maajabu yake wakati mkutano wa hadhara 
uliohutubiwa na Ridhiwani Kikwete katika Kata ya Kiwangwa
 Mwenyekiti mpya wa Serikali ya 
Kijiji cha Kiwangwa, Kata ya Kiwangwa, akifungua rasmi mkutano wa 
hadhara uliohutubiwa na Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete 
katika Kata ya Kiwangwa ambapo pamoja na kusikiliza kero zao 
aliwashukuru wananchi kwa kumchagua mwaka jana.
 Mkazi wa Kiwangwa Shabani Dume akiuliza swali kwa kumtaka Mbunge Ridhiwani asaidie kuwepo dampo katika Kijiji cha Kiwangwa
 Kassim Makelele wa Kata ya Kiwangwa akimuomba Mbunge Ridhiwani kununua Ambulance kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Kiwangwa
 Diwani wa Viti Maalumu Tarafa ya 
Msata, Rehema Mno akielezea kwa wananchi jinsi alivyoshiriki kutatua 
kero za wananchi katika Kata ya Kiwangwa.,
 Ridhiwani akiteta jambo na Diwani wa Kata ya Kiwangwa, Yahaya Ramadhani  wakati wa mkutano huo
 Sehemu ya umati uliohudhuria katika mkutano huo
 Ridhiwani akihutubia katika 
mkutano huo ambapo aliwaambia viongozi wa Tanesco kuhakikisha wana 
peleka haraka umeme wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA) katika Kijiji cha 
Kiwangwa
 Meneja wa Tanesco Wilaya ya Chalinze, Julius Doyi akiwaambia wananchi wa Kiwangwa kuwa umeme utaingia hapo mwezi huu.
 Meneja wa Mamlaka ya Usafi wa 
Maji Safi na Taka wa Chalinze,Injinia Christer Mchomba akielezea kwa 
wananchi mikakati mbalimbali ya kuharakisha upatikanaji wa maji katika 
Kata ya Kiwangwa.
 Ridhiwani akaimkabidhi Bondia Idd Pialali gloves 20 kwa ajili ya kuendeleza mchezo wa ngumi katika Kata ya Kiwangwa
Ridhiwani akimkabidhi mpira mmoja 
wa wa manahodha wa timu mbalimbali katika Kata ya Kiwangwa  kwa ajili ya
 kuendeleza soka katika kata hiyo.
No comments:
Post a Comment