Mbunge Mtemvu kulia, akielekeza jambo.
……………………………………………………………………………………………
Na Khamisi Mussa
WANAFUNZI
 10 kutoka vyuo Vikuu vya Bufalo na Empire vya Marekani wamewasili 
nchini kwa ziara ya mafunzo kwa mwaliko wa Mbunge wa Jimbo la Temeke, 
Abbas Mtemvu.
 Akizungumza
 na waandishi wa habari Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere 
Dar es Salaam leo mara baada ya kuwapokea wanafunzi hao ambao 
wanaongozwa na Profesa Dan Nyaronga, Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu 
alisema wageni hao watapata fursa ya kutembelea miradi mbalimbali iliyopo katika Jimbo lake pamoja na Kampuni yake ya Bravo Job Centre Agency Ltd.
Alisema
 mbali ya kutembelea jimbo la Temeke pia watatembea Taasisi ya 
Wajasiriamali ya Poverty Fighting Tanzania iliyopo Tandika na mkoa wa 
Mara, katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Kitenga ambayo waliichangia
 sh.milioni 1.5, Miradi ya Maendeleo ya Kanisa la Anglikana Dayosisi ya 
Tarime Magharibi, Shule ya Bohare Community Development na Hospitali ya Mkoa wa Mara ambapo watajifunza masuala ya afya.
Alisema
 baada ya ziara ya mkoa wa Mara watatembelea mkoa wa Kilimanjaro na 
mbuga za wanyama na kuwa wataondoka nchini Januari 21, 2015.
No comments:
Post a Comment