Mratibu
 Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la 
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez 
akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Bi. Anne Rose Nyamubi mara 
baada ya kuwasili ofisini kwake kwa ajili ya mazungumzo kabla ya 
kuelekea kwenye kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum wakiwemo 
walemavu wa ngozi cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga.
Na mwandishi wetu, Shinyanga
MKUU 
wa wilaya ya Shinyanga AnneRose Nyamubi ameomba jamii ya watanzania 
kusaidia kupatikana kwa zahanati katika kituo cha kulelea watoto 
walemavu cha Buhangija ili kupunguza adha wanazopata watoto hao katika 
huduma za afya.
Kauli
 hiyo ameitoa katika mazungumzo na mwandishi wa habari hizi ambaye 
alifika katika kituo hicho akiambatana na ujumbe wa Umoja wa Mataifa 
uliokuwa ukiongozwa na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na
 mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, 
Alvaro Rodriguez.
Nyamubi
 amesema kwamba ingawa hospitali ya mkoa ina dirisha kwa ajili ya 
matibabu ya watoto hao,wakati mwingine inakuwa shida daktari maalumu 
anayehusika anapokuwa hayupo.
Aidha
 alisema kwa namna watoto hao walivyo wanahitaji huduma ya karibu ya 
kitiba ambayo inawezekana kama kituo hicho kingekuwa na zahanati yake.
Mkuu
 wa Wilaya ya Shinyanga, Bi. Anne Rose Nyamubi akiwa kwenye mazungumzo 
na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa 
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
 aliyeambatana na Mshauri wa masuala ya haki za binadamu kutoka ofisi 
kwake, Bi. Chitralekha Massey ( wa pili kulia kwake) pamoja na Mtaalam 
wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu
 (wa pili kushoto). Wengine katika picha ni Afisa Elimu Sayansikimu, 
Beatrice Mbonea (wa kwa kulia), Afisa Elimu Msingi wa manispaa ya 
Shinyanga, Bi. Pudensiana Magnus (katikati kulia), Mkurugenzi wa 
manispaa ya Shinyanga, Festo Kang’ombe pamoja na Msaidizi wa Mkuu wa 
Mkoa wa Shinyanga, Bw. Shadrack Kengese.
Kituo
 hicho kilichoanzishwa mwaka 2010 kwa ajili ya watoto walemavu 
wasiosikia na wasiiona kwa sasa kinapokea watoto wenye alibnizim ambao 
wanaokabiliwa na ujahiri dhidi ya maisha yao.
Kwa 
mujibu wa mkuu huyo wa wilaya kituo hicho ambacho serikali hutenga 
bajeti kwa ajili ya wanafunzi 50 wasiosikia na kuona, sasa kina watoto 
wenye albinism 247 ambao hawako katika bajeti na wanaishi kutokana na 
misaada ya watu mbalimbali.
Alisema
 kwamba watoto wenye albinism wanahitaji huduma za tiba za karibu zaidi 
kutokana na mazingira yanawazunguka na dirisha pekee katika hospitali ya
 mkoa halitoshi kwani wakati mwingine wanalazimika kukaa kwenye foleni 
kama wagonjwa wengine na hili halipendezi.
Aidha
 alisema kituo hicho cha Buhangija kwa sasa ni kidogo kuzingatia na 
uwingi wa wanaohitaji msaada na hivyo serikali inatafuta eneo jingine 
kwa ajili ya kujenga kituo.
Mazungumzo
 yakiendelea ndani ya ofisi za Mkuu wa mkoa wa Shinyanga zinazokaimiwa 
na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Bi Anne Rose Nyamubi.
Kufurika
 kwa watoto hao wenye ulemavu kunatokana na tishio la maisha yao hasa 
ukanda wa Ziwa ambapo familia zao zimewakimbiza kituoni hapo kwa ajili 
ya usalama wao.
Aidha
 Mkuu huyo wa wilaya amesema kwamba kituo hicho hakina bajeti na kutaka 
wasamaria wema kuendelea kuchangia ili watoto hao waendeshe maisha ya 
kawaida.
Naye 
Mratibu wa Mashirika ya Umoja Mataifa yaliyopo nchini, Alvaro Rodrigues 
amesema kwamba Umoja wa Mataifa utaendelea kusaidia kituo hicho na 
kuwataka wanaotunzwa hapo kutoacha kuishi kama watoto kwani ndio tunu 
waliyonayo kwa sasa.
Aidha
 alisema kwamba anauchukua wimbo waliouimba ambao unazungumzia machungu 
ya maisha yao na kwenda kuwaeleza watu wengine ili nao washiriki katika 
kubadilisha hali ya kuogofisha na kuleta usalama.
Mkurugenzi
 Mtendaji wa shirika la UNDER THE SAME SUN, Vicky Ntetema alijumuika 
kwenye mazungumzo hayo. Pichani akifafanua jambo kwa Mratibu Mkazi wa 
mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la 
Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (hayupo pichani) 
kuhusiana na changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wenye ulemavu wa 
ngozi nchini.
Alisema wao (UN) wamefika katika kituo hicho kuona watoto wanavyoishi na watafanya nini kuwasaidia.
Aliwataka Watanzania kuhakikisha wanakomesha machungu ya albino hao na kuishi nao kama watu wengine wa kawaida.
Aidha
 Mratibu huyo alipata nafasi ya kuzungumza na Binti wa miaka 19 Masabu 
masuka ambaye amejifungua mwaka jana kituoni hapo bila msaada wa wauguzi
 baada ya kulazimika kuondoka kwao akiwa mjamzito kukwepa mauaji dhidi 
ya albino yaliyofanyika Mei mwaka jana wilayani Bariadi.
Binti huyo alifika kituoni hapo na kaka zake watatu ambao wote ni maalbino kama yeye.
Mkuu
 wa wilaya ya Shinyanga, Bi Anne Rose Nyamubi katika picha ya pamoja na 
ugeni kutoka ofisi za Umoja wa Mataifa Tanzania na Shirika la UNDER THE 
SAME SUN.
Mkuu
 wa wilaya ya Shinyanga, Bi Anne Rose Nyamubi akiwasalimia watoto wenye 
ulemavu wa ngozi wanaolelewa kwenye kituo cha Buhangija Jumuishi 
kilichopo mkoani Shinyanga kabla ya kumtambulisha Mratibu Mkazi wa 
mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la 
Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (hayupo pichani).
Mratibu
 Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la 
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) 
akizungumza na watoto wenye ulemavu wakiwemo wa ngozi (hawapo pichani) 
wanaolelewa kwenye kituo cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani 
Shinyanga alipofanya ziara ya kutembelea kituo hicho. Katikati ni 
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania 
Hoyce Temu na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Bi. Anne Rose 
Nyamubi.
Mratibu
 Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la 
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akitoa 
zawadi ya maziwa kwa watoto wenye ulemavu wa ngozi wanaolelewa kwenye 
kituo cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga.
Mtaalam
 wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce 
Temu akishiriki kwenye zoezi la kugawa zawadi kwa watoto hao.
Mratibu
 Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la 
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Mshauri
 wa masuala ya haki za binadamu kutoka ofisi ya Mratibu huyo, Bi. 
Chitralekha Massey wakiendelea na zoezi la kugawa zawadi kwa watoto hao.
Mratibu
 Mkazi huyo Bw. Alvaro Rodriguez akiwasaidia watoto hao kufungua biskuti
 alizowapekea kama zawadi alipotembelea kwenye kituo hicho.
Mkurugenzi
 Mtendaji wa shirika la UNDER THE SAME SUN, Vicky Ntetema akieleza jambo
 kwa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa 
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
 (kulia) alipokuwa akikagua mazingira ya kituo hicho na kuona ni jinsi 
atawasaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili kituo hicho.
Pichani ni jiko la kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wakiwemo wa ngozi cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga.
Mwalimu
 Mkuu wa shule ya watoto wenye maalum ya Buhangija Jumuishi, Peter Ajali
 akitoa maelezo ndani ya moja ya mabweni kituoni hapo kwa Mratibu Mkazi 
wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo 
la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) na kushoto 
ni Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la UNDER THE SAME SUN, Vicky Ntetema.
Mwalimu
 Mkuu wa shule ya watoto wenye maalum ya Buhangija Jumuishi, Peter Ajali
 akimwonyesha baadhi ya sehemu ambazo hazisakafiwa ndani ya mabweni 
kituoni hapo Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na 
mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, 
Alvaro Rodriguez.
Baadhi
 ya matandiko wanayotumia watoto hao wenye mahitaji maalum kulali kwenye
 sakafu ambayo haijasakafiwa na pia kutokana na uhaba wa mabweni 
inawalazimu kubanana na kulala bila uhuru.
Bweni
 lililojengwa na Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred linalohudumia 
watoto 48 ambalo linahitaji kumaliziwa ili watoto hao nao waweze kulala 
mahali pazuri.
Mratibu
 wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini,Alvaro Rodrigues akizungumza na
 binti wa miaka 19 ambaye ni mlemavu wa ngozi na kutosikia, Masalu 
Masuka ambaye anaishi katika kituo cha watoto walemavu cha Buhangija 
baada ya kukimbia kwao Bariadi kukwepa wauaji wa albino. Binti huyo 
alijifungua mtoto wake akiwa kituoni hapo bila msaada wa muuguzi. Kituo 
hicho kinahitaji msaada wa kujengewa zahanati. (Picha na Zainul wa Mo 
Blog)
Mratibu
 Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la 
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akicheza 
mpira ambao ni moja ya zawadi alizozitoa kwa watoto wenye ulemavu wa 
ngozi wanaolelewa kwenye kituo cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani 
Shinyanga alipofanya ziara ya kukitembelea kituo hicho kinachokabiliwa 
na changamoto mbalimbali na kuwaahidi kuwasaidia huku akiwashirkisha na 
wadau wengine wa maendeleo. Kushoto mwenye kofia ni Khassan Khamis na 
kulia ni Emmanuel Deus.
Mratibu
 Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la 
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiendelea
 kucheza mpira na kufurahi na watoto hao wenye ulemavu wa ngozi.
Mratibu
 Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la 
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiwa 
amembeba mtoto mwenye ulemavu wa ngozi Ghoke Maliwa anayelelewa kwenye 
kituo cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga alipofanya ziara
 ya kukitembelea kituo hicho juzi mkoani humo.
Mratibu
 Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la 
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisoma 
ujumbe unaosema “DREAM BIG” kwenye T-shirt ya mtoto Agnes Kabika mwenye 
ulemavu wa ngozi anayelelewa kwenye kituo cha Buhangija Jumuishi 
alipofanya ziara ya kutembelea kituo hicho.
Mshauri
 wa masuala ya haki za binadamu kutoka ofisi ya Mratibu huyo, Bi. 
Chitralekha Massey akibadilishana mawazo na binti anayefanya shughuli za
 kujitolea Claire Grubbs kutoka nchini Marekani aliyepiga kambi kwenye 
kituo cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga.


No comments:
Post a Comment