Mwenyekiti
wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu ambaye pia ni Mbunge wa
Jimbo la Lushoto Dkt. Henry Shekifu akisalimiana na wakandarasi wa
Makampuni ya Aasleaff na Bam International wanaojenga barabara ya
Laela-Sumbawanga kwa kiwango cha lami. Kamati hiyo ya Bunge ipo Mkoani
Rukwa kwa zaira ya siku mbili ambapo itakagua miradi mbalimbali ikiwemo
barabara za Tunduma-Ikana-Laela, Laela-Sumbawanga, Sumbawanga-Kasanga,
Bandari ya Kasanga na Miundombinu ya Anga ambapo wataona eneo la Kisumba
lililotengwa tangu mwaka 1984 kwa ajili ya kujengwa uwanja mkubwa wa
ndege na pia wataona uwanja wa ndege wa Sumbawanga.
Mwenyekiti
wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu ambaye pia ni Mbunge wa
Jimbo la Lushoto Dkt. Henry Shekifu wa tatu kushoto Meneja wa Tanroad
Mkoa wa Rukwa Florence Kabaka na wajumbe wengine wa Kamati hiyo ya Bunge
wakishika udongo uliochanganywa na Cement na kushindiliwa ikiwa ni
mojawapo ya hatua kuelekea ujenzi wa kiwango cha lami katika barabara ya
Laela Sumbawanga eneo la kyanda walipokagua ujenzi wa barabara hiyo.
Wafanyakazi
wa Kampuni ya Aasleff na Bam International wakiendelea na ujenzi wa
barabara hiyo. Mpaka sasa kilomita zaidi ya 10 zimeshawekwa lami ya
majaribio na kazi nzima katika barabara hii ya Laela - Sumbwawanga
imeshafikia asilimia 37 hadi kukamilika kwake.
Umwagiliaji kuimarisha ujenzi ukiendelea.
Wafanyakazi wakiendelea kuchapa kazi, hapo wakiondoa kokoto kwa ajili ya kuweka surface nyingine.
Mhe.
Shekifu na Kamati yake wakiangalia moja ya eneo lililoanza kupata nyufa
katika baadhi ya maeneo yaliyoanza kuwekwa lami. Mwenyekiti huyo
alimuasa Mkandarasi huyo mambo matatu moja ikiwa ni kupata taarifa rasmi
yenye uhakika kutoka kwao kuwa ni lini mradi huo utakamilika ili
wawatangazie wananchi wenye kiu kubwa na barabara hizo. Pili wahakikishe
ubora wa barabara hizo unazingatiwa ikiwa ni pamoja na kukabiliana na
tatizo la nyufa zilizoanza kujitokeza katika baadhi ya maeneo
yaliyowekwa lami. Na mwisho ni kuhakikisha suala la fidia kwa wananchi
wanaostahiki linakamilika kuepusha usumbufu wowote ule.
No comments:
Post a Comment