TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, July 28, 2014

Manji aunda jeshi jipya, Bin Kleb ajitoa

By KHATIMU NAHEKA 
Abdallah Bin Kleb.  
-====================================
Kwa kushirikiana na Makamu wake, Clement Sanga, Manji ameunda kamati hiyo kwa mamlaka aliyonayo kupitia azimio la Mkutano Mkuu uliofanyika Januari 20 ambao ulimpa madaraka ya kufanya mabadiliko ya kamati ya utendaji atakavyojisikia.
MWENYEKITI wa Yanga, Yusuf Manji, amevunja Kamati ya Utendaji na mara moja ameitangaza kamati mpya ambayo haina jina la Abdallah Bin Kleb.
Kwa kushirikiana na Makamu wake, Clement Sanga, Manji ameunda kamati hiyo kwa mamlaka aliyonayo kupitia azimio la Mkutano Mkuu uliofanyika Januari 20 ambao ulimpa madaraka ya kufanya mabadiliko ya kamati ya utendaji atakavyojisikia.
Kwa mujibu wa taarifa ya Manji iliyosomwa na Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu, kamati mpya itaanza kazi Agosti Mosi ambapo kila mjumbe aliyeteuliwa amepewa kazi maalumu za kusimamia. Ni tofauti na ilivyokuwa katika kamati aliyoivunja.
Wajumbe wa kamati mpya ni Abubakar Rajabu ambaye amepewa kazi ya kusimamia mradi wa ujenzi wa Jangwani City, Salum Mapande (Sheria na Utawala Bora),George Fumbuka (Uundwaji wa shirika) na Abbas Tarimba (Mipango ya Uratibu).
Wengine ni Isaac Chanji na Seif Ahmed ‘Seif Magari’ (Uendelezaji wa Michezo), Musa Katabaro (Mauzo na Biashara), Mohamed Bhinda (Ustawishaji matawi), David Sekione ‘Seki’ (Uongezaji Wanachama) na Mohamed Nyenge (Utangazaji wa Habari, Taarifa na Matangazo).
Wakati huohuo, kamati mpya iliyotangazwa haina jina la Bin Kleb ambaye awali alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, lakini mwenyewe amesema aliomba kutojumuishwa kwenye kamati mpya.
Mmoja wa mabosi wa Yanga, alisema Bin Kleb ameomba kupumzika ili aweze kushughulikia mambo yake binafsi.
“Si kwamba Mwenyekiti ana tatizo na Bin Kleb, walizungumza kwa muda mrefu na kukubaliana apumzike. Bin Kleb ndiye aliyeomba apumzike,” alisema bosi huyo.

No comments:

Post a Comment