TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, January 14, 2015

Mradi wa M-pesa wanufaisha Vijana wa Misungwi.

unnamed
Mwenyekiti wa kikundi cha Vijana Songambele akifurahia jambo pamoja na maafisa kutoka wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo walipokuwa wakizungumza mara baada ya kuwa tembelea hivi karibuni (wapili kushoto) ni Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji na Tathimini Bibi. Verdiana Mushi. Picha na Anitha Jonas – Maelezo Misungwi
……………………………………………………………………………………..
Na: Anitha Jonas, Maelezo – Misungwi
Vijana wa kikundi cha Songambele katika Kata ya Misungwi Soko Kuu wameishukuru Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kwa kuwapatia mkopo wa shillingi milioni uliosaidia kuanzisha Mradi wa wakala wa M-pesa katika Wilaya ya Misungwi na Kwimba. Mwenyekiti wa kikundi hicho Bw. Josephat Mabele alitoa shukrani kwa niaba ya kikundi chake alipotembelewa na maafisa kutoka Wizara ya Habari ,Vijana, Utamaduni na Michezo katika eneo la Mradi huo kwa ajili ya kufanya tathimini na ufuatiliaji kwa Wilaya ya Misungwi, “Mradi huu wa M-pesa umetusaidia kwa kiasi kikubwa kwani tunaweza kupata faida ya zaidi ya laki tano kwa mwezi kupitia mradi huu na hivyo kufanya kipato chetu kukuwa kwa kiasi kikubwa na hata kubadili hali zetu za maisha”,alisema Bw. Mabele. Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji na Tathimini Bi. Verdiana Mushi kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo aliwapongeza vijana hao na kuwaasa kuwa makini katika utekelezaji wa mradi huo kwani biashara ya fedha matapeli ni wengi hivyo ni vyema kumdai kitambulisho kila mteja anayeenda kwa ajili ya kupata huduma. Bibi Mushi amewata wanakikundi kuwa na mwongozo mzuri utakaowasaidia kufanya marejesho ya mkopo huu kwa wakati ili vijana wenzao nao waweze kunufaika na fursa ya kukopeshwa mkopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana. Kwa upande wake Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Eliakim Mtawa aliwashauri vijana hao kuendeleza umoja katika kikundi kufikia malengo waliyokusudia na kutoa elimu kwa vijana wenzao ili waweze kukomboka kama wao walivyojikomboa. Aidha Afisa Vijana kutoka Halmashauri ya Misungwi Bw. Allan Jackson alisema kuwa Halmashauri ya Misungwi kwa kushirikana na Misungwi Vijana Saccoss itaendelea kusimamia vijana hao katika miradi yao na kuhakikisha wanarejesha mkopo kwa wakati kwa ajili ya kupatiwa vikundi vingine vya vijana katika Halmashauri yake.

No comments:

Post a Comment