Kwanza
 kabisa Napenda kuchukua nafasi hii Kumshukuru sana Mwenyezi Mungu 
Mwingi Wa Rehema Kwa Kuweza Kunijalia Uwezo,Nguvu na Afya na Bahati Pia 
ya Kuweza Kufika Mwaka 2014, Siwezi Kujidanganya Wala Kudanganya Kuwa 
nimefika Hapa Leo Mnamo tarehe 1 Jan 2014 Kwa ujanja wangu au uwezo 
hapana Nimefika hapa Kwa Neema Na Rehema Zake Mwenyezi Mungu Mwingi wa 
Rehema, Na pIa sio Kwasababu ameniwezesha Kuuona na kuingia leo tarehe 1
 Jan 2014 basi mimi ni mwema, msafi na mtiifu sana mbele zake kuliko 
wengine hapana Ila Ni Kwa Neema na Makusudi yake Pia Wapo waliopenda 
kuiona Siku kama ya Leo Lakini kwa mapenzi yake Muumba Hawakuweza kufika
 na Pia wapo walioweza Kufika lakini wakiwa sio wazima Kiafya Na Sio 
kwamba wao ni wakosaji sana mbele za Mungu hapana Bali yote hayo Hutokea
 Kwa Makusudi yake na 
Mipango yake Pia.
Tuna
 kila sababu ya Kumbuomba Mwenye Mungu Mwingi wa Rehema Kila Dakika 
itupitayo na Sio Kusubiri Mwaka Mpya ndio Tumuombe, Tuna kila sababu ya 
kufanya kila siku iendayo kwake basi iwe ni Mwaka Mpya Kwake Kwa Kuomba,
 Kusali na KUmwabudu maana ni yeye Pekee ndiye Muweza wa Kila Jambo.
Napenda
 Kuchukua Nafasi hii Kuwatakia Watanzania wote na Dunia Nzima wakiwemo 
Wazazi Wangu, Ndugu zangu, kaka zangu, Dada zangu ,Wajomba, Mashangazi, 
Mama Wadogo, baba Wadogo, Marafiki zangu, Watembeleaji wa Blogu zenu 
wote, Marafiki zenu, Ndugu zenu, Bila kuwasahau Maadui zangu Wote maana 
na wao pia ni sehemu ya mimi kupata mafanikio madogo sana maana 
Usijisifie Kuwa Unaweza kukimbia Sifa pia Kilichokukimbiza au 
aliyekukimbiza pia…Kwa Kuweza Kufika Mwaka 2014 wakiwa na afya na wazima
 wa afya, Na Hata wale waliokuwa wagonjwa Basi Mwenyezi Mungu Awatie 
Nguvu ili waweze kupona na Kurejea majumbani Mwao wakitokea 
Mahospitalini kwaajili ya Kuungana na Familia zao pia.
Mwaka
 2014 umeanza ikiwa ndio siku ya Kwanza kabisa ya Mwaka 2014, Tuzidi 
Kumuomba Mungu Mwingi wa Rehema Azidi Kutuepusha na Kutupigania katika 
Vita ya Kiroho dhidi ya Mwovu Shetani na Mawakala zake kama CHuki, Roho 
Mbaya, Majungu, Masimango, Uchawi, Na vingine vingi vya namna hiyo.
Vilevile
 napenda Kuchukua nafasi Hii Kuwashukuru wote kwa kuendelea Kuwa nami 
katika Kipindi hiki chote cha Mwaka 2013 na naomba tuendelee 
kushikamana, Kupendana, Kuombeana Mazuri na yenye heri na Kuweza Kufika 
Pale tulipojiwekea malengo yetu tena Kwa Mwaka 2014.
Namwomba
 Pia Mwenye Mungu Mwingi wa Rehema Azidi kunipa Nguvu, Afya , Hekima na 
Busara katika Kazi zote za halali nizifanyazo na hatimaye kuweza 
kufanikiwa hadi pale apendapo yeye nifike.
Mwisho
 Nachukua Nafasi hii Kuwatakia Wote Heri ya Mwaka Mpya 2014. Tufanye 
kazi Kwa Bidii na Tuzidi Kumuomba Yeye Kwa Ni yeye ndie atupaye Nguvu na
 kututia uwepesi wa Kila Jambo
No comments:
Post a Comment