Mwimbaji
 wa muziki wa injili Rose Muhando akiimba na kucheza jukwaani wakati wa 
tamasha la Krismas lililofanyika leo kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid 
jijini Arusha leo na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi wa jiji hilo, 
ambapo waimbaji mbalimbali wamepanda jukwaani na kukonga nyoyo za 
mashabiki wao wakiwemo Bony Mwaitege, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, 
Edson Mwasabwite, Tumaini Njole, The Voices, Victoria Singerls, mwimbaji
 wa kimataifa wa muziki wa injili kutoka nchini Zambia Ephraim Sekereti 
na wengine wengi. 
 
 
Mwimbaji Bony Mwaitege akiruka jukwaani wakati alipokuwa akiimba. 
Wakurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion wakijadili jambo 
 
Wakurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion wakijadili jambo 
 
Askofu mkuu wa makanisa ya
 Calvary Asemblies of God , Dunstan Maboya akitoa neno katika tamasha la
 Krismas  kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid leo huku akiwa ameambatana 
na mchungaji mwenzake, kushoto ni Alex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya 
Msama Promotion 
 
 
wimbaji
 wa kimataifa wa muziki wa injili kutoka nchini Zambia Ephraim Sekereti 
akifanya vitu vyake jukwaani katika tamasha la Krismas jijini Arusha 
leo. 
Kundi la The Voices likifanya vitu vyake jukwaani.
 
 
 
 
 
 



No comments:
Post a Comment