TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, January 23, 2012

RAISI KIWETE, MIZENGO PINDA WAONGOZA MAZISHI YA ALIYEKUWA MBUNGE WA ARUMERU MASHARIKI

Rais Dk. Jakaya Kikwete akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Mbunge wa Arumaru Marehemu Jeremiah Sumari katika mazishi yaliyofanyika mkoani Arusha leo huku rais Jakaya akiongoza mamia ya waombolezaji.
NA GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWE- ARUSHA
ALIYEKUWA Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Bw Jeremiah Sumari amezikwa jana kijijini kwake Akheri wilayani Meru Mkoani hapa na mazishi hayo kuongozwa na Raisi wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya kikwete, pamoja na waziri mkuu Bw Mizengo Pinda.
Akiongea na waombolezaji waliofika katika eneo hilo la Akheri waziri Pinda alisema kuwa viongozi mbalimbali wa Serikali wanatakiwa kuwa mfano wa kuigwa kama alivyokuwa Bw Sumari
Bw Pinda alieleza kuwa kiongozi kama kiongozi anatakiwa kuwa na sifa ambazo zitamfanya jamii imlkumbuke mara zote na sifa hizo zinatakiwa kuwa ni miongoni mwa sifa nzuri na zenye kulijenga taifa.
“hii ni safari ya Bw Sumari lakini sote tunatakiwa kuhakikisha kuwa tunaweka hazina hapa duniani, na kuwa na sifa nzuri na zenye kupendeza, kwa kuwa kifo ni msingi wa kila mwanadamu hapa duniani”aliongeza bw Pinda.
Pia aliitaka familia ya Marehemu Sumari kuhakikisha kuwa haioni mzigo kwa kuondokewa na Baba yao na badala yake wahakikishe kuwa wanaendelea kumtegemea zaidi Mungu katika mambo yao ikiwa ni pamoja na kufuata Mambo mazuri ambayo yalikuwa yanafutwa na Bw Sumari.
Katika hatua nyingine viongozi mbalimbali ambao waliongoza ibada hiyo ya Mazishi walisema kuwa kwa sasa jimbo la Arumeru Mashariki limepoteza Mbunge wake kwa maana hiyo ni lazima taratibu za kumtafuta Mbunge huyo zifanyike wakati utakapofika lakini wagombe wanatakiwa kuwa makini na kuachana na tabia ya uchakachuaji wa matokeo
Walibanisha kuwa endapo kama zoedzi la uchakachuaji wa matokeo katika jimbo hilo ni wazi kuwa watakuwa wanaweka jimbo hilo mashakani kabisa hali ambayo itachangia matatizo mbalimbali juu ya jimbo hilo.
“tunatangaza rasmi kabisa kuwa hapa hamna masuala ya kuachakachua matokeo kwa maana hiyo uchaguzi utakaokuja ni lazima matokeo yawe ya halali kwa maslahi ya jimbo hili”waliongeza wachungaji hao.
Aidha nao viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) walisema kuwa wao kama chama kupitia kwa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo walikuwa na ahadi nyingi dhidi ya jimbo hilo ambapo ahadi hizo zilikuwa na lengo la kusaidia jamii.
Walisema kuwa ahadi za mbunge huyo kwa jimbo hilo ziko palepale na zitatekelezwa kwa mujibu wa sheria ya chama hicho kwa eneo hilo la Arumeru Mashariki ili kuweza kupambana na changamoto mbalimbali.

Na Mwandishi wa Jeshi la Polisi-Zanzibar Makamanda wa Jeshi la Polisi Zanzibar wameahidi kuendelea kushirikiana na Wadau wa vyombo vya Habari hapa nchini kwa kutoa taarifa sahihi na kwa wakati muafaka ili kuwawezesha wananchi kupata haki yao ya kikatiba ya kupashwa habari.
Afisa Habari wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, amesema kuwa ahadi hiyo imetolewa na Makamanda wa Polisi kutoka mikoa mitatu ya Unguja waliokuwa wakishiriki katika Mafunzo ya Uhusiano wa Polisi na Vyombo vya Habari yaliyokuwa yakifanyika kwenye chuo cha Polisi Zanzibar.
Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hayo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, ACP Aziz juma Mohammed, amesema Polisi na Wanahabari ni watu wanaotegemeana kitaaluma na kwamba kazi ya Polisi isingetambulika kwa urahisi kwa raia kama sio juhudi za vyombo vya Habari.
Kamanda Azizi amesema ili kuwawezesha Waandishi wa Habari kutangasa habari kwa usahihi ni lazima Polisi nao wasiwe na kigugumizi katika kutoa taarifa zinazohitajika kwa waandishi.
Amesema kutoa taarifa sahihi na kwa wakati muafaka, kunaondoa uvumi ama minong’ono ya taarifa za kweli zilizokosa ufafanuzi kutoka kwa msemaji wa eneo husika.
Naye Kamaba wa Polisi wa Mkoa wa Kusini Unguja ACP Augost Uromi, ameitaja mifano michache ya jinsi Polisi wanavyowahitaji Waandishi wa Habari kuwa ni pamoja na kusaidia kueneza mpango wa Polisi Jamii na Ulinzi Shirikishi jambo ambalo lingewawia Polisi vigumu kumfikia mwananchi moja mmoja kumjulisha juu ya dhana hiyo.
Amesema Vyombo vya Habari vinapotumika vizuri, huwawezesha watu wengi kupata habari moja na kwa wakati mmoja na hivyo kuna umuhimu mkubwa kwa Polisi kuendelea kushirikiana kwa dhati na vyombo vya Habari na kuwaona ni wadau muhimu.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kaskazini Unguja ACP Ahmada Abdallah, amesema kuwa ili kuepuka waandishi kuandika taarifa zisizo sahihi ni vema kila Kamanda kuwa tayari kutoa taarifa za matukio kila yanapotokea.
Akitoa mada wakati wa mafunzo hayo, Mkuu wa Chuo cha Polisi Zanzibar SSP Ramadhan Mungi, aliwaambia walishiriki wa hao kuwa ili kuepuka upotoshwaji wa taarifa ni muhimu kila taarifa inayotolewa kwa waandishi wa Habari iwe ya maandishi.
Awali akifungua Mafunzo hayo, Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa, alisema kuwa Mafunzo hayo yameandaliwa ili kuwawezesha Maafisa wa Polisi kujua namna ya utayarishaji na usambazaji wa taarifa kwa vyombo vya Habari (Press Release) na jinsi ya kuandaa na kufanya mikutano ya moja kwa moja na waandishi wa habari. (Press Conference).
Mafunzo hayo ya siku mbili ambayo yalikuwa yakifanyika kwenye Chuo cha Polisi Zanzibar, (Zanzibar Police Academy) yamewashirikisha Kamakanda wa Polisi wa mikoa yote ya Unguja, Wakuu wa Upelelezi na Maafisa Wanadhim kutoka Mikoa ya Mjini Magharibi, Kusini na Kaskazini Unguja pamoja na Maafisa Waandamizi wa Polisi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Zanzibar.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi Daraja la Mingumbi lililopo Wilaya ya Kilwa, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya Mkoa wa Lindi jana Januari 22, 2012. Kushoto ni mkewe, Mama Zakhia Bilal (kulia) ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovic Mwananzila. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Msimamizi wa kituo cha afya cha Kitomanga, Dkt. Issa Michenje, kuhusu jengo jipya la Kituo cha afya cha Kitomanga, Lindi Vijijini, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Lindi jana Januari 22, 2012. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwasalimia wananchi baada ya kuweka Jiwe la Msingi katika jengo la Kituo cha Afya cha Kitomanga lililopo Lindi Vijijini wakati akiwa katika zaiara yake mkoa wa Lindi jana, januari 22, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Moahammed Gharib Bilal, akizungumza na wananchi wa Kitomanga, baada ya kuzindua rasmi jengo la Kituo cha afya cha Kitomanga, Lindi Vijijini, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Lindi jana Januari 22, 2012. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi, alipozindua Daraja la Mingumbi lililopo Kilwa, wakati akiwa kwenye ziara yake ya Mkoa wa Lindi jana, Januari 22, 2012. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovic Mwananzila.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi Jengo jipya la Bwalo la Shule ya Sekondari ya wasichana Ilulu, iliyopo Kilwa, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya mkoa wa Lindi jana Januari 22, 2012. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovic Mwananzila.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya Ilulu, baada ya kuzindua rasmi Jengo la Bwalo la shule hiyo, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya Mkoa wa Lindi jana Januari 22, 2012.

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fissoo akionesha Sheria namba 4 ya mwaka 1976 ya Utengenezaji wa Filamu na Michezo ya Kuigiza kwa waandishi wa habari ambao hawapo pichani wakati akitoa ufafanuzi wa kuhusu sheria hyo kwa vyombo vya vya habari leo jijini Dares Salaam.
Benjamin Sawe
Maelezo
Dar es Salaam
Wasanii wa Filamu na Michezo ya Kuigiza wameshauriwa kuzisoma nyaraka mbalimbali za Bodi ya Filamu ili wajue sheria na kanuni zinazohusu tasnia ya hiyo.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Joyce Fissoo alipokuwa akitoa ufafanuzi juu ya Sheria namba 4 ya Utengenezaji wa Filamu na Michezo ya Kuigiza ya mwaka 1976.
Akifafanua juu ya sheria hiyo, Bi Fissoo alisema ndiyo inayoendelea kutumika mpaka sasa na kukanusha tuhuma zilizosambazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa ya uwepo wa matumizi ya sheria mpya.
“Hakuna Sheria mpya ya Filamu na Michezo ya Kuigiza iliyotungwa, Sheria inayoendelea kutumika ni ile ya mwaka 1976 bali kilichofanyika ni utekelezaji wa kanuni za sheria ya filamu na michezo ya kuigiza ambapo mchakato wake ulianza mwaka 2011.
Akizungumzia juu ya malalamiko ya baadhi ya wasanii kushindwa kuhimili kulipa ada ya Sh. 500,000(laki tano) Bi. Fissoo alisema kifungu cha 8 cha sheria hiyo kinampa Waziri mwenye dhamana husika kutoa msamaha wa malipo kwa msanii mchanga atakayeshindwa kulipa kiasi cha fedha hizo.
“Ada wanayolipa wasanii ya Sh.500, 000 (laki tano) ipo toka siku za nyuma ambapo Sheria namba 4 ya Filamu na Michezo ya kuigiza inampa mamlaka Waziri husika kutoa msamaha kwa msanii mchanga atakayeshindwa kulipa ada hiyo”.alifafanua.
Alisema kwamba msamaha wa ada ya sh. 500,000 utatatolewa pale tu msanii atakapotoa taarifa kwa Waziri husika na mara baada ya kujiridhisha ndipo msamaha utatolewa na kutangazwa kwenye gazeti la Serikali.
Amewashauri wasanii wa Filamu kuwa Wazalendo kwa kutengeneza filamu zenye maadili ya Mtanzania na si kutengeneza Filamu zenye maudhui ya kimagharibi.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki mchezo wa kuvutana kwa kamba na wafanyakazi wa Sahara Communications Ltd, wakati wa Bonanza la wafanyakazi hao kwenye ufukwe wa ziwa Victoria jijini Mwanza.
Nape na baadhi ya wafanyakazi wa sahara wakishangilia baada ya kundi lao kuwashinda wengine katika kuvuta kamba.
Wanawake wakishindana kuvuta kamba katika bonaza hilo.
Hawa ndiyo vimwana wa Sahara Communication hebu wacheki katika pozi hii ya picha wakishangilia.

Mkuu wa kitengo cha Mauzo cha Vodacom m-pesa Franklin Bagalla(kushoto)akimsisitiza jambo Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya kifedha ya PTF Mary Likwelile,wakati wa semina ya chama cha Taasisi za kifedha (TAMFI)iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania mahususi kwa ajili ya kunufaika na huduma ya m-pesa,semina hiyo iliandaliwa na Vodacom Tanzania jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa kitengo cha Mauzo cha Vodacom m-pesa Franklin Bagalla(kulia)akisikiliza swali kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Tanzania Association of Microfinance Association(TAMFI)Joel Mwakitalu wakati wa semina mahususi kwa ajili ya Chama cha Taasisi za kifedha kuweza kunufaika na huduma ya m-pesa,semina hiyo iliandaliwa na Vodacom Tanzania jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa semina ya Taasisi za kifedha(TAMFI)wakimsikiliza Mkuu wa kitengo cha Mauzo cha Vodacom m-pesa Franklin Bagalla wakati wa semina hiyo mahususi kwa ajili ya taasisi hizo kunufaika na huduma ya Vodacom m-pesa,iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
kuu wa kitengo cha Mauzo cha Vodacom m-pesa Franklin Bagalla na Meneja wa Vodacom m-pesa Magesa Wandwi wakisikiliza swali kutoka kwa mratibu wa Taasisi za kifedha wa Mkoa wa Arusha Hamisi Shelukamba wakati wa semina ya Taasisi za kifedha (TAMFI)iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania mahususi kwa ajili ya kunufaika na huduma ya m-pesa,semina hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam
Baadhi ya washiriki wa semina ya Taasisi za kifedha nchini(TAMFI)wakifatilia mada iliyokuwa inatolewa na Mkuu wa kitengo cha Mauzo cha Vodacom m-pesa Franklin Bagalla(hayupo pichani)iliyohusu huduma ya Vodacom m-pesa,Semina hiyo iliandaliwa na Vodacom Tanzania jijini Dar e s Salaam.

Mwandishi wetu
NYOTA imeanza kung’ara kwa mbunifu wa mavazi anayekuja juu jwa kasi nchini, Doreen Estazia na lebo yake ya Estado Bird baada ya kupata kualikwa kuhudhuria mkutano wa kujadili masuala ya Uchumi duniani (World Economic Forum) utakaonza kesho mjini Devos –Klosters, Uswisi.
Estazia ambaye mwishoni mwa mwaka jana aliibuka na mavazi yaliyojulikana kwa jina la What’s Your Freedom (WYF?) kwa ajili ya kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania alisema kuwa amealikiwa kama mjasiliamali katika masuala ya ubunifu wa mavazi na atakuwa chini ya Global Shapers.
Alisema kuwa hii ni faraja kubwa kwake kwani kipaji chake ndicho kimempa nafasi hiyo na kuwa mbunifu wa kwanza nchini tokea taifa hili lizaliwe kushiriki katika mkutano huo mkubwa.
Alifafanua kuwa setka ya ubunifu wa mavazi inanulikana kimataifa kwani mbali ya kupromoti nchi nje ya mipaka na hasa masuala ya vivutio vya utalii kwa upande wa mavazi.
“Nashukuru kupata nafasi hii na nitaiwakilisha vyema Tanzania, hii ni fursa pekee ya kujitangaza kimataifa na hasa ukizingatia kuwa nimeanza kujihusisha na masuala ya ubunifu mwaka mmoja uliopita,” alisema Estazia kabla ya kuondoka juzi usiku.
Alisema kuwa ameanza kupata mwanga wa mafanikio na lengo lake kubwa ni kufikia hatua ya juu kabisa katika masuala ya ubunifu wa mavazi na wala si viginevyo.
“Sina malengo ya kuishia hapa hapa katika fani hii, nataka dunia inifahamu kupitia ubunifu wa mavazi, mkutano wa Uswis ni moja ya njia ya kufikia lengo kwani unawajumuisha pia wakuu wan chi mbali mbali duniani,” alisema.

Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia timu ya Bunge wameomba kucheza mechi maalumu dhidi ya Twiga Stars kabla ya kuwasilisha mchango wao kwa timu hiyo.
Benchi la Ufundi la Twiga Stars kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limekubali kucheza mechi hiyo ambayo itakuwa ni ya maonesho tu ambapo baada ya kumalizika ndipo Wabunge watakabidhi kile walichopanga kutoa kwa timu.
Mechi hiyo itafanyika Alhamisi (Januari 26 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume uliopo Ofisi za TFF kuanzia saa 10 kamili jioni.
Twiga Stars na Namibia zitapambana Jumapili (Januari 29 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ikiwa ni mechi ya marudiano kuwania tiketi ya kufuzu kwa fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) zitakazofanyika Novemba mwaka huu nchini Equatorial Guinea.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kikagua ujenzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tekinolojia cha Nelson Mandela kilichopo Arusha wakati alipokitembela Januari 22, 2012.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Lindi mjini, Salum Baruani, wakati alipowasili kwenye Shule ya Sekondari Mnolela, lindi kwa ajili ya kuzindua Jengo la Utawala la shule hiyo, jana januari 21, 2012, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Lindi
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia ngoma ya asili wakati alipowasili kwenye shule ya Sekondari ya Mnolela, alipofika kuzindua Jengo la Utawala la shule hiyo, akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Lindi jana, Januari 21, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa ikiwa ni ishara ya kuweka jiwe la Msingi katika jengo jipya la Utawala la Shule ya Sekondari Mnolela, iliyopo kijiji cha Luhokwe, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Lindi jana Januari 21, 2012
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Lindi, kuelekea kukagua ujenzi wa jengo la Bweni la wasichana shule ya Sekondari ya Kineng’ene, akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Lindi, jana Januari 21, 2012
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Uwanja wa Fisi Lindi jana Januari 21, 2012, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Lindi

No comments:

Post a Comment