TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, January 24, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AANZA ZIARA YA MKOA WA TANGA LEO, AKAGUA UKUTA WA KUZUIA MAJI YA BAHARI PANGANI

Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi Jengo la Ofisi ya Idara ya Maji, lililopo Wilaya ya Pangani, wakati alipoanza ziara yake ya Mkoa wa Tanga leo, Januari 24, 2012. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa (kushoto) ni Mkurugenzi wa Maji wa wilaya hiyo, Mohamed Hamis.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu ukuta huo unaozuia maji ya Bahari unaobomoka kutokana na mabadiliko ya Tabia nchi na kutishia amani ya wakazi wa maeneo hayo. Pangani Kivukoni.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya Viongozi wa Wilaya ya Pangani wakati akitoka kukagua ukuta wa kuzuia maji ya Bahari unaobomoka Pangani Kivukoni.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia ukuta unaozuia maji ya Bahari eneo la Pangani Kivukoni, unaozidi kubomoka kutokana na kujengwa miaka 100 iliyopita na kutishia amani kwa wakazi wa maeneo hayo. Makamu wa Rais ameanza ziara yake ya Mkoa wa Tanga leo Januari 24, 2012.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, amekutana na watendaji wa Wizara Afya, Ikulu Mjini Zanzibar leo,katika mpangilio wake wa kuzungumza na kila Wizara ya Serikali ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na watendaji wa Wizara Afya katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar jana,katika mpangilio wake wa kufanya mazungumzo na kila Wizara ya Serikali. Picha na Ramadhan Othman IKULU.

KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma(PAC), imeagiza kwamba sheria inayoruhusu Mamlaka ya Nishati na Madini(EWURA) kulipa mishahara ya watumishi wa Baraza Ushauri na Watumaji la Nishati na Madini (EWURA CCC) ibadilishwe ili baraza hilo liweze kufanya kazi ipasavyo.
Hayo yalisemwa leo na Makamu Mwenyekiti wa PAC, Deo Filikunjombe wakati akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye ofisi ndogo za Bunge jijini Dares Salaam kuhusu shughuli zilizofanywa na kamati yake , ambapo alisema baraza hilo hesabu zake zinakwenda vizuri.
“Baraza hili hesabu zake ni nzuri , lakini halifanyi kazi ipasavyo kwa kuwa halimtendei kazi ipasavyo liko pamoja na EWURA tumeagiza sheria ibadilishwe ili liweze kufanya kazi kwa kuzingatia pande zote,” alisema Filikunjombe.
Makamu Mwenyekiti huyo alishauri kuwa ni vyema mishahara hiyo ilipwe na wizara husika ili baraza hilo lifanye kazi bila kuegemea upande mmoja.
Akizungumzia kuhusu upandaji wa umeme kwa asilimia 40 alihojia upanda kwa sababu zipi je mlaji wa chini wamemsikiliza wanasemaje, hivyo alisema haitakuwa sahihi ikiwa hakusikilizwa.
Aliongeza kuwa baraza hilo pia linatakiwa kuacha kulipa malipo ya kila baada ya miaka mitano mtumishi anapostaafu badala yake yawe katika mfumo ya mifuko ya hifadhi ya jamii, ikiwemo kuwaingiza watumishi wake katika Mfuko wa Bima ya Afya ili kuepuka utumiaji wa risiti za malipo ya matibabu.
Alitaka baraza hilo kutumia fedha kulingana na bajeti yake.
Wakati huohuo Filikunjombe alisema kamati hiyo imemfukuza mwakilishi wa Shirika Hodhi la Mali za Umma (CHC) kwa kuwa ni mtendaji wa chini hawawezi kuzungumza naye hivyo wanamtaka Ofisa Mtendaji Mkuu.
Alisema mwakilishi aliyetumwa ni Ofisa Uhusiano ambayo ameitumwa na Kaimu Mkurugenzi.

Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
Kuanzishwa kwa mkakati wa kitaifa wa mabadiliko ya Tabia nchi kutaiwezesha na kuiongezea uwezo nchi ya Tanzania kushirikiana na mataifa mbalimbali katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchini yanayoendelea kuikumba dunia.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Mazingira, Ofisi ya makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi wakati akifungua mkutano wa wadau wa mazingira kujadili mkakati wa kitaifa wa mabadiliko ya Tabia nchi.
Amesema hivi sasa mabadiliko ya tabia nchi yameleta athari kubwa duniani ikiwemo ongezeko la gesi joto angani jambo ambalo linahitaji juhudi za mtu mmoja mmoja, vikundi, Taasisi na Jumuiya za kimataifa kushirikiana kwa pamoja kuinusuru dunia kutokana na athari za mabadiliko hayo.
“ Tanzania na watanzania wote kwa ujumla watapata fursa ya kushiriki katika fursa za miradi ya kupunguza gesi joto kupitia sekta binasfi hasa fursa za miradi ya kupunguza gesi joto inayoanzishwa nchini na kuwawezesha watanzania kupata fedha huku wakiendelea kufanya shughuli zao za kila siku”
Amefafanua kuwa mkakati huo wa kitaifa wa mabadiliko ya Tabia nchi utaisaidia nchi ya Tanzania kushiriki katika masuala mbalimbali ya kimataifa na kuiwezesha kuwa na msimamo kama nchi kupinga vitendo vyote vinavyofanywa na mataifa mbalimbali yaliyoendelea kiviwanda ambayo yanachangia kwa kiwango kikubwa ongezeko la gesi joto duniani.
Pia amefafanua kuwa licha ya mkakakati huo kuanzishwa kwa mara ya kwanza kwanza nchini utaiwezesha Tanzania kuwa ushirikiano na nchi nyingine za Afrika, jumuiya mbalimbali za kimatifa ndani na nje ya bara la Afrika na kuongeza kuwa ukamilishwaji wa mkakati huo utaiwezesha nchi kupanga na kuamua masuala mbalimbali yahusuyo mabadiliko ya Tabia nchi.
Aidha amefafanua kuwa sanjari na kuwepo mkakati huo ambao ni mkubwa masuala ya mazingira yataendelea kuongozwa na mkakati wa kitaifa wa mwaka 2006 na ule wa 2007 unaotoa mwongozo kuhusu masuala mbalimbali ya mazingira yakiwemo uzuiaji wa uchafuzi na uharibifu wa vyanzo vya maji katika mito na uharibifu wa misitu na mazingira.
Kwa upande wake mshiriki wa mkutano huo kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam Prof. Richard Kangalawe amefafanua kuwa mabadiliko ya tabia nchi yanendelea kuathiri kwa kiasi kikubwa uchumi wan chi yetu na hata kutishia maisha ya kila siku.
Amezitaja baadhi ya changamoto ambazo Tanzania kwa sasa inakabiliana nazo kutokana na mabadiliko ya Tabia nchi kuwa ni pamoja na ukame katika baadhi ya maeneo, mafuriko yanayojitokeza katika maeneo mbalimbali nchini kutokana na mvua zinazonyesha kwa muda mfupi na ongezeko la magonjwa mbalimbali.
“Kama tunavyoona kuna dalili mbalimbali ambazo zinaonyesha kuwa hali ya mabadiliko ya tabia nchi imekuwa kubwa sana tofauti na miaka 30 iliyopita na inaliathiri taifa hasa baadhi ya matukio mbalimbali yaliyotokea hivi karibuni ikiwemo mvua kubwa zilizonyesha na kusababisha mafuriko katika maeneo mbalimbali nchini na kusababisha madhara makubwa katika jiji la Dar es salaam.

Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (kushoto) akiwekeana saini na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Motherland Industries Limited kutoka India Bw, V. K. Sood (Kulia) uwekaji saini wa mikataba mitatu ya utafiti wa mafuta nchini, umefanyika leo jijini Dar es Salaam, (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO)
Kamishna Msaidizi wa Nishati kutoka Wizara ya Nishati na Madini Bw, Prosper Victus (alisimama mbele na Kabrasha) akitoa maelezo ya awali wakati wa uwekaji wa saini mikataba mitatu ya utafii wa mafuta kutoka kampuni za nje leo wakati wa hafla hiyo kwenye jengo la Wizara ya hiyo jijiji Dar es Salaam. (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).
Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (kulia) akifafanua jambo wakati wa uwekaji saini wa mikataba mitatu ya uatafiti wa mafuta kutoka kampuni za nje jijini leo DSM (Kulia) ni Kamishna Msaidizi wa Nishati (Petroleum na Gas ) Bw, Prosper Victus, (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
Waziri wa Nishati na Madini Wiliam Ngeleja (kushoto) akibadilisha hati za makubaliano ya utafiti wa mafuta nchini na Mkurugenzi Mtendaji wa kampun i ya Petrobras kutoka Brazil Bw, Samuel Bastos de Miranda (kulia) , hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es Slaam wakati wa hafla ya uwekaji saini wa mikataba mitatu ya utafiti wa mafuta wa kampuni kutoka nje, (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).
Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (katikati) akiweka saini mkataba wa utafiti wa mafuta nchini kwa kampuni tatu kutoka nje, (kushoto) ni Mkurugenzi mtendaji wa TPDC Bw, Yona Killagane na (kulia) Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Matherland industries LTD kutoka India, Bw. V.K. Sood .(kulia). Mkataba huo umewekwa saini leo kwenye jingo la Wizara ya Nishati na Madini, (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na watendaji wa Wizara ya Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati, Ikulu Mjini Zanzibar,katika mpangilio wake wakuzungumza na kila Wizara ya Serikali ya Zanzibar,katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo. Picha na Ramadhan Othman IKULU.
Baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na watendaji hao Ikulu Mjini Zanzibar,katika mpangilio wake wakuzungumza na kila Wizara ya Serikali ya Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akisalimiana na ujumbe wa Mabalozi wa Tanzani Nchi za Nje,ambao wanakwenda nchi mbali mbali kiwakilisha Tanzania,walipofika kumuaga Rais Ikulu Mjini Zanzibar.(24 Jan 2012)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akisalimiana na ujumbe wa Mabalozi wa Tanzani Nchi za Nje,ambao wanakwenda nchi mbali mbali kiwakilisha Tanzania,walipofika kumuaga Rais Ikulu Mjini Zanzibar.(24 Jan 2012) Picha na Ramadhan Othman IKulu.

Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kupitia kitengo chake cha utatuzi wa migogoro (Dispute Resolution Chamber- DRC) limeagiza klabu ya Yanga kumlipa mchezaji John Njoroge sh. 17,159,800 ikiwa ni fidia kwa kuvunja mkataba wake kinyume cha taratibu.
Uamuzi huo wa DRC chini ya Jaji Theo van Seggelen ambaye ni raia wa Uholanzi ulifanywa Desemba 7 mwaka jana jijini Zurich, Uswisi na kutumwa TFF kwa njia ya DHL, Januari 17 mwaka huu.
Njoroge ambaye ni raia wa Kenya aliwasilisha kesi yake FIFA kupinga Yanga kuvunja mkataba alioingia wa kuichezea timu yao kinyume na makubaliano. Mchezaji huyo hivi sasa anachezea timu ya Tusker ambayo ni mabingwa wa Kenya.
Yanga ina siku nne za kukata rufani kupinga uamuzi huo kuanzia tarehe iliyoupokea kama inataka kufanya hivyo. Klabu hiyo inatakiwa iwe imeshamlipa Njoroge ndani ya siku 30 tangu ilipopokea uamuzi huo. Ikishindwa kulipa ndani ya muda huo, itatozwa riba ya asilimia 5 kwa mwaka ya fedha hizo.
Ikiwa Yanga itashindwa kulipa ndani ya muda huo vilevile suala hilo litafikishwa mbele ya Kamati ya Nidhamu ya FIFA kwa hatua zaidi.
Powered by Sorecson : Creation de site internet

Kiingilio cha chini kwa mechi ya kufuzu kwa fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) kati ya Twiga Stars na Namibia itakayochezwa Jumapili (Januari 29 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kitakuwa sh. 2,000.
Kiwango hicho ni kwa washabiki kwa viti vya bluu na kijani. Viti hivyo kwa pamoja vinachukua jumla ya watazamaji 36,693 kwenye uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua washabiki 60,000.
Pia kutakuwa na kiingilio cha watoto wenye umri wa chini ya miaka 10 ambacho ni sh. 1,000. Watoto watakaotumia tiketi hizo wanatakiwa kuingia uwanjani wakiwa na wazazi au walezi wao.
Viingilio vingine kwa mechi hiyo ni sh. 3,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 5,000 kwa VIP B na C n ash. 10,000 kwa VIP A.
Namibia inatarajia kuwasili nchini Ijumaa (Januari 27 mwaka huu) saa 12.45 jioni kwa ndege ya South Africa Airways.

Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imefanya marekebisho madogo kwenye ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom kutokana na Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kutumika kwa sherehe za kitaifa za kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mechi namba 111 kati ya Toto Africans na African Lyon ambayo kwa mujibu wa ratiba ilikuwa ichezwe Februari 5 mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza sasa itachezwa Aprili 18 mwaka huu.
Mabadiliko hayo yamefanyika baada ya wamiliki wa Uwanja wa CCM Kirumba, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kueleza kuwa watautumia kwa sherehe za kuzaliwa chama chao, hivyo hautakuwa na nafasi kwa Februari 4, 5 na 6 mwaka huu.
Uamuzi huo umesababisha pia mabadiliko kwa mechi nyingine mbili. Mechi namba 168 kati ya Villa Squad na African Lyon iliyokuwa ichezwe Aprili 18 mwaka huu Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam, sasa itachezwa Aprili 22 mwaka huu.
Pia mechi namba 170 kati ya Azam na Toto Africans iliyokuwa ichezwe Aprili 29 mwaka huu jijini Dar es Salaam sasa imerudishwa nyuma hadi Aprili 26 mwaka huu ambayo ni Sikukuu ya Muungano.

Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Mazingira,Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi akizungumza na wadau wa mazingira kutoka Taasisi mbalimbali,wizara na wadau kutoka nchi wahisani wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau hao unaojadili mabadiliko ya Tabia nchi na mkakati wa kitaifa kuhusu mabadiliko ya Tabia nchi leo jijini Dar es salaam. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
Mshauri wa masuala ya mabadiliko ya Tabia nchi kutoka Idara ya Kimataifa ya Maendeleo (DFID) nchini Tanzania Bi. Magdalena Banasiak (kushoto) akizungumzia athari za mabadiliko ya Tabia nchi duniani na mchango wa wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi katika kuhakikisha kuwa athari za mabadiliko ya tabia nchi zilizoanza kujitokeza zinadhibitiwa.
Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Mazingira,Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi akiwasilisha mada kuhusiana na mabadiliko ya Tabia nchi na ripoti ya tafiti ya athari za kimazingira iliyofanyika katika baadhi ya maeneo yakiwemo Zanzbar, Mbeya, Tanga, Manyara, Shinyanga na Mwanza leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wadau wa Mazingira kutoka ndani na nje nchi wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa mkutano wa wadau wa mazingira kuhusu mkakati wa kitaifa kuhusu mabadiliko ya Tabia nchi leo jijini Dar es salaam.
Wadau wa Mazingira kutoka, Taasisi mbalimbali,wizara na wadau wa mazingira kutoka nchi wahisani wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano unaojadili Mkakati wa Kitaifa kuhusu mabadiliko ya Tabia nchi leo jijini Dar es salaam.

Ayoub Mzee at the Africa Union Summit to attend the 18th ordinary session of the assembly of heads of state and governments
The advent of the African Union (AU) can be described as an event of great magnitude in the institutional evolution of the continent. On 9.9.1999, the Heads of State and Government of the Organisation of African Unity issued a Declaration (the Sirte Declaration) calling for the establishment of an African Union, with a view, inter alia, to accelerating the process of integration in the continent to enable it play its rightful role in the global economy while addressing multifaceted social, economic and political problems compounded as they are by certain negative aspects of globalisation.
The main objectives of the OAU were, inter alia, to rid the continent of the remaining vestiges of colonization and apartheid; to promote unity and solidarity among African States; to coordinate and intensify cooperation for development; to safeguard the sovereignty and territorial integrity of Member States and to promote international cooperation within the framework of the United Nations.
Indeed, as a continental organization the OAU provided an effective forum that enabled all Member States to adopt coordinated positions on matters of common concern to the continent in international fora and defend the interests of Africa effectively.
Through the OAU Coordinating Committee for the Liberation of Africa, the Continent worked and spoke as one with undivided determination in forging an international consensus in support of the liberation struggle and the fight against apartheid.

HII siyo bahati nasibu wala Bingo bali ni msaada wa kumuwezesha Mchungaji Deogratius Mosha wa Kanisa la Elishadai Gospel Ministry katika kumuwezesha kujikwamua kiuchumi kwenye Kanisa lake, hii ni sehemu ya mkakati wa Kanisa la Amri kuu za Mungu (Akuzamu) lililoko Jijiji Dar es salaam katika jengo la IPS,linalofundisha watu masuala ya uchumi na kuwawezesha kwa mahitaji mbalimbali ambapo tukio hili lilifanyika katika semina ya uchumi iliyofanyika kwenye ukumbi wa Nadd's uliko Salender Bridge juzi (picha na Salesi Malula)
Na salesi Malula
Mchungaji Edward Amri wa huduma ya Amri Kuu za Mungu (AKUZAMU) amewapiga marufuku waumini wake kuacha kuilaumu Serikali kwani haisaidii chochote katika maisha yao na kufanya hivyo ni kinyume na Neno la Mungu.
Ameyasema hayo alipokua akifundisha Neno la Mungu katika ibada ya Jumapili, ambapo aliwaasa wakristo kufuata Kanuni ya Neno la Mungu, ili waweze kufanikiwa katika kila eneo na kuepuka kuilaumu serikali kila mara, jambo ambalo haliwezi kuleta majibu katika maisha yao ya Kila siku.
Alisema ifikie mahali Watanzania wajiulize nini wataifanyia nchi yao kwani sisi kama Kanisa lazima tuwe Baraka kwa Taifa na siyo kugeuka wapinzania kwa kuilaumu serikali; kinachotakiwa kila Kanisa liwe na utaratibu wa kuwasaidia waumini wake kwa kuwapa mafundisho ya namna ya kujikwamua kiuchumi, likiwepo suala la kuwahamasisha waweze kujiajiri ili waweze kuisaidia serikali katika kutoa ajira na kulipa kodi kwa usashihi.
“Kazi ya Kanisa ni kuisaidia serikali na siyo kuipinga na kuwatengeneza watu wake yaani waumini kuwa raia wema wenye kuipenda nchi yao likiwepo suala la kuwakwamua watu kiuchumi kwa kuwafundisha mafundisho sahihi ya uchumi katika ufalme wa Mungu, kama ambavyo kanisa letu linafanya ambapo muda si mrefu sisi tutakuwa Baraka katika Taifa kwani waumini wetu wengi wataajiri na watakuwa na walipakodi wazuri katika nchi yetu”.
Akiongea kwa kujiamini alisema kwa sasa uchumi wa dunia nzima umekwama na sababu yake ni kwamba ni vigumu sana uchumi wa mfumo huu kufaulu kwa sababu hauna mbadala, yaani ziada kwani masomo hayo ya uchumi yanayofundishwa shuleni miaka 20 iliyopita ndio hayo hayo yanafundishwa hivyo wachumi wetu hawawezi kuwa na la ziada zaidi ya kujifunza masomo ambayo wenzao waliyagundua zamani na ndio maana hadi hivi sasa hawawezi kutoa majibu ya kuboresha maisha ya wananchi.
Akitoa mfano alisema kwa sasa nchini kwetu hatuna vitu ambavyo tumegundua. Kwa mfumo wa uchumi wa kwenye makaratasi hauwezi kutoa majibu kwani hata hao wachumi endapo masomo yangekuwa na hatimiliki nadhani sisi tusingekuwa na kitu kwani masomo hayo tunakopi kutoka kwa wenzetu ambapo hatuwezi kuwa na mbadala na ndio maana unaweza kukuta tunao wasomi wengi wa uchumi wasipoajiriwa hawawezi kuishi wanachanganyikiwa maana hawana mbadala
Akieleza mikakati ya Kanisa lake amesema wao wameamua kuisaidia serikali badala ya kuilaumu kwa kuwaelimisha waumini wao masuala ya uchumi katika ufalme wa Mungu kwa kutumia Neno la Mungu, pamoja na kuwahamasisha juu ya umuhimu wa kujiajiri ili waweze kuwaajiri wengine.
Akijitolea mfano yeye alisema kabla hajaanza kumtumikia Mungu alijiajiri kwa kufungua biashara ambapo miaka hivi sasa anao wafanyakazi wasiopungua mia moja wanaofanyakazi katika biashara zake hivyo amekua msaada kwa serikali kwa kuipunguzia kero ya ajira kwani ameajiri na analipa kodi serikalini hivyo amekua Baraka kwa nchi.
Mbali na hilo amekuwa na mkakati wa kuwahamasisha wale aliowaajiri kutojisahahu badala yake nao wafungue biashara zao nao waweze kuajiri watu wengine kwani ifikie hatua tuipunguzie mzigo serikali badala ya kuilaumu.
Amekemea tabia ya baadhi ya watumishi pamoja na waumini kuilaumu serikali kwa kusema eti inasababisha hali ngumu jambo ambalo amesema si kweli kwani mazingira ya sasa karibu nchi zote zimekwama ni wakati wa Kanisa kuisaidia serikali kwa kuwafundisha waumini Neno la Mungu kwa usahihi pamoja na kuwasaidia kujiajiri badala ya kutumia muda mwingi kuilaumu serikali jambo ambalo si sahihi.
Tangu mwaka 2012 Kanisa la Akuzamu chini ya kiongozi wake Mchungaji Edward Amri limeanzisha kampeni kabambe kuisaidia serikali kwa kuiombea pamoja na kuwahamasisha waumini wake kujiajiri na kuwaajiri wale ambao bado hawana ajira ambapo pia limekuwa likitoa mafundisho ya uchumi kila siku katika ukumbi wa IPS Jijini Dar es salaam na kila mwezi, ambapo mwezi ujao linatarajia kuendesha semina kubwa itakayofanyika katika ukumbi wa Nadd’s ulioko salender bridge jijini Dar es salaam tarehe ishirini na tano mwezi ujao ambapo wengi wamekuwa wakihudhuria na mara baada ya mafundisho wengi wamebadilika katika ufahamu wao na wameanza kuchukua hatua ya kujiajiri.

No comments:

Post a Comment