TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, March 7, 2015

TAARIFA YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA BIOMETRIC VOTER REGISTRATION (BVR) KATIKA KATA TISA (9) ZA HALMASHAURI YA MJI WA MAKAMBAKO KUANZIA TAREHE 23/2/2015 HADI 3/3/2015


imagesTume ya Taifa ya Uchaguzi imeanza rasmi zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura baada ya kukamilika kwa maandalizi muhimu ya Uboreshaji wa Daftari, ikiwemo manunuzi ya vifaa na upatikanaji wa fedha kutoka Serikalini.
Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, tofauti na Uboreshaji wa Daftari hilo kwa Awamu zote za Chaguzi zilizopita, linafanyika kwa kutumia teknolojia mpya ya Biometric Voter Registration (BVR). Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lilianza kufanyika katika Kata tisa (9) za Halmashauri ya Mji wa Makambako katika Vituo 54 vilivyowekwa katika Mitaa na Vitongoji, kuanzia tarehe 23/2/2015 katika Kata za Kitisi, Kivavi, Lyamkena, Maguvani, Majengo, Makambako, Mji Mwema, Mlowa na Mwembetogwa. Tume ililenga kuandikisha Wapiga Kura 32,370 kwa mujibu wa taarifa za Ofisi ya Takwimu za Sensa ya Idadi ya watu ya mwaka 2012. Tume ililenga kuandikisha kwa siku jumla ya watu 1,850. Hata hivyo mara baada ya uandikishaji kuanza idadi ya Wapiga Kura waliokuwa wanajitokeza iliendelea kuwa kubwa na kuongezeka kila siku ambapo kulikuwa na misururu mirefu ya watu waliojitokeza kujiandisha katika Vituo vyote vya Uandikishaji. Tume ilivuka malengo yaliyowekwa ya Uandikishaji kutokana na kujitokeza kwa wingi kwa Wapiga Kura waliofika katika Vituo vya Uandikishaji kila siku kwa Kata zote tisa (9) za Mji wa Makambako ambazo zilikuwa zinaandikisha Wapiga Kura. Idadi ya Wapiga Kura waliojitokeza na kuandikishwa kwa kila siku katika Kata tisa (9) za Mji wa Makambako ilikuwa kama ifuatavyo:- i. Tarehe 23/2/2015 Tume iliandikisha Wapiga Kura 3,014; ii. Tarehe 24/2/2015 Tume iliandikisha Wapiga Kura 4,727; iii. Tarehe 25/2/2015 Tume iliandikisha Wapiga Kura 5,301; iv. Tarehe 26/2/2015 Tume iliandikisha Wapiga Kura 6,354; v. Tarehe 27/2/2015 Tume iliandikisha Wapiga Kura 6,731; vi. Tarehe 28/2/2015 Tume iliandikisha Wapiga Kura 6,545; vii. Tarehe 1/3/2015 Tume iliandikisha Wapiga Kura 6,906; viii. Tarehe 2/3/2015 kutokana na Watu waliokuwa wanajitokeza kujiandikisha kuendelea kupungua, Tume iliandikisha Wapiga Kura 4,662; na

No comments:

Post a Comment