TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, March 7, 2015

WAZIRI NYALANDU AKUTANA NA WAZIRI MWENZAKE WA KENYA ITB BERLIN

laz1Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akiwa na Waziri wa Biashara na Utalii wa Kenya Bibi Phylis Kandie mara baada ya mazungumzo yao.

laz2Mh. Waziri Nyalandu akihojiwa katika banda la Tanzania na mwandishi wa habari wa kituo cha Televisheni cha Check inn cha Qatar Bw. Tajamul Hussain kuhusu utalii wa Tanzania kwa ujumla.
laz3MKurugenzi wa kampuni ya usafirishaji watalii ya Zara tours kutoka Moshi Tanzania bibi Zainabu akizungumza na Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalndu alipotembelea banda la Tanzania kujionea namna waoneshaji wa Tanzania wanavyoitangaza Tanzania katika maonesho ya ITB berlin.
laz4Waziri wa Biashara na Utalii wa Kenya Mh. Phylis Kandie akisakata rhumba na Waziri wa Maliasili na utalii wa Tanzania Mh. Nyalandu katika banda la Tanzania.
…………………………………………………………………..
Na: Geofrey Tengeneza – Berlin Ujerumani Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu amekutana na waziri mwenzake wa Biashara na Utaliiwa Kenya Bibi Phylis Kandie katika banda la Kenya na kuwa na mazungumzo yanayohusu ushirikiano wa nchi mbili katika sekta ya Utalii. Mazungumzo hayo hayakuwa rasmi hivyo hayakuhudhuriwa na wandishi wa habari Aidha Wiziri Nyalandu alitembelea banda la Tanzania na kuzungumza na washiriki wa maonesho ya ITB kutoka makampuni mbalimbali washiriki hao kwa ambapo amewapongeza kwa kuitangaza vema Tanzania katika maonesho hayo.

No comments:

Post a Comment