TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, March 7, 2015

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA KWA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA IRINGA

Mwenyekiti  wa CCM mkoa  wa Iringa  Jesca Msambatavangu  akionyesha kanuni  za  uongozi na maadili za CCM leo  alipozungumza na  wanahabari mkoa  wa Iringa
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa  Jesca Msambatavangu  akizungumza na  wanahabari leo  ofisi ya  chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC()
Wanahabari  Iringa  wakimsikiliza mwenyekiti wa CCM mkoa
…………………………………………………………………………….
ILIYOJITOKEZA BAADA YA MAAMUZI MBALI MBALI
KUFANYIKA NA KUTANGAZWA KUHUSU MAADILI YA UONGOZI.
UTANGULIZI
Mtakumbuka kuwa tarehe 2/3/2015 kuna kauli ambayo ilitolewa na Katibu wa wilaya ya Mufindi Ndugu Mtaturu.
 Ambayo ilielekeza baadhi ya hatua
zilizochukuliwa na Chama cha Mapinduzi kwa baadhi ya wanachama wetu,
ikiwa ni pamoja na kufukuzwa uanachama kwa baadhi ya makada wetu.
 Akiwemo Shukuru Luhambati, Clara Shirima na Hosea Kaberege. Swala hili
limeamusha malalamiko na mjadala miongoni mwa wanaCCM na wapenzi na
wakereketwa wa CCM. Kila mtu akiwa na mtizamo wake kuhusu swala hili,
ambalo pia kimepelekea kuamsha malumbano katika vyombo mbali mbali vya
habari.

Lakini pia kumetokea wasi wasi mkubwa kwa baadhi ya wanachama ambao
walihojiwa na kamati za maadili na kuwa na uvumi pia kuwa watafukuzwa
au kunyang’anywa uanachama.

 Hiyo pia imeleta uvumi kuwa Mimi Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa
pia nimesimamishwa uanachama na kuvuliwa nafasi zote za uongozi.
Moja, Sitofahamu iliyojitokeza kwa wale walioachishwa UANACHAMA:
(Shukuru Luhambati, Clara Shirima na Hosea Kaberege)
Kwa mujibu wa Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM. Toleo la 2010
zilizotolewa na Halshauri Kuu ya Taifa. Fungu la Nne (8vi) pg 30
linalohusu adhabu mbali mbali kwa makosa yanayohusu ukiukwaji wa
Maadili.
Inasema katika kipengele hicho:
(vi) Kuachishwa Uanachama:
MwanaChama anayegundulika ana makosa ya Itikadi, yanayoathiri Uhai wa
Chama, au ambaye ameshindwa huko nyuma kujirekebisha hata baada ya
Karipio, wala haonyeshi dalili za kuweza kujirekebisha hata akipewa
muda zaidi, basi Kamati ya Usalama na Maadili ya Taifa inaweza
kupendekeza mbele ya Kamati Kuu mwanachama huyo aachishwe UANACHAMA.
Ikiridhika, Kamati Kuu itapeleka shauri hilo mbele ya Halmashauri Kuu
ya Taifa kwa uamuzi wa mwisho.
(a) Adhabu ya kuachishwa Uanachama itatangazwa hadharani.
Pia Fungu la Tatu linalohusu: WAJIBU WA KUSIMAMIA TABIA, MWENENDO NA VITENDO VYA MWANACHAMA NA KIONGOZI; Ni wa vikao vya Chama cha Mapinduzi vya Halmashauri kuu na Kamati zake za Siasa kwa kila ngazi kama ilivyoanishwa kikatiba.
Kwa swala la leo hapa: Ibara ya 93(8), (14) na (15), Halmashauri Kuu
ya CCM Mkoa:-…….(14) Kumwachisha au kumfukuza Uanachama Mwanachama ye
yote endapo itaridhika kwamba tabia na mwenendo wake vinamwondolea
sifa za uanachama.
 Mwanachama anayeachishwa au kufukuzwa uanachama
anaweza kukata rufaa kwa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa.
Hivyo basi, hakuna sababu yakuwa na hofu au mashaka.
Wale ambao
wanadhani hawajatendewa haki wanahaki ya kukataa rufaa vikao vya juu
zaidi, kama Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa.
Pili, Kuhusu Mwenyekiti wa CCM Mkoa kusimamishwa Uongozi sio kweli.
 Ibara 93 (15) fungu la tatu. Halmashauri Kuu ya Mkoa; Inaweza
Kumwachisha au Kumfukuza Uongozi kiongozi ye yote ambaye uteuzi wake
wa mwisho unafanywa na Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa.
Pia,Ibara 95(7) Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya Mkoa;
Kumsimamisha uongozi kiongozi ye yote wa ngazi ya wilaya endapo
itaridhika kwamba tabia na mwenendo wake vinamwondolea sifa za
uongozi

Isipokuwa kwamba haitakuwa na uwezo wa kumsimamisha uongozi
kiongozi ambaye uteuzi wake wa mwisho haukufanywa na Halmashauri Kuu
ya CCM Mkoa.
Kwa nafasi yangu mimi kama Mwenyekiti wa Mkoa siwezi kusimamishwa
uongozi na ngazi ya Mkoa. Hata pia kwa nafasi ya Diwani lazima
ipelekwe vikao vya ngazi ya Taifa.
  Ingawa wilaya ya Iringa Mjini kupitia Katibu wake Zongo Lobe Zongo
wamenipa Adhabu mimi Mwenyekiti wa Mkoa kwa Kupewa Adhabu ya Onyo
Kali. Taratibu nyingine zitafuatwa kwa mujibu wa vikao


 Nina toa maelekezo pia kwa Kamati za Maadili zote katika ngazi zote za
Mkoa wa Iringa kuzingatia kanuni, Katiba na maelekezo ya Chama katika
utekelezaji wao wa Kazi zao za Kamati ili kutoviyumbisha vikao vya
maauzi vya Chama.
Pia ili kuondoa mgongano unaweza ukajitokeza kati ya
viongozi, wanachama na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi kwa ujumla wake.
Kwa mujibu wa Kanuni za uongozi na maadili toleo la 2012; fungu la nne
7(1)…”Katika kusimamia maadili ya viongozi wa CCM wakati wo wote wa
utekelezaji wa kanuni hizi, ..Kamati ya Usalama na maadili katika
ngazi inayohusika (mkoa) itazingatia Katiba ya CCM na Kanuni zingine
za CCM zitakazo kuwepo wakati huo, pamoja na maelekezo mengine ya
msingi yatakayokuwa yametolewa na Halmashauri Kuu ya Taifa
Ninawasisitiza kuzingatia zaidi; Kanuni za Uongozi na Maadili fungu la Nne 7(4)ii-kinachohusu Tuhuma: Kinasema Uchambuzi wa tuhuma hizo utafanywa kwa kutumia njia mbali mbali
pamoja na mashahidi watakaoweza kupatikana.
Na endapo itadhihirika kwamba tuhuma zina uzito, mtuhumiwa atatitwa
mbele ya kikao cah Kamati ya Usalama na Maadili ya ngazi inayohusika,
kama ni lazima, ili apate kuhojiwa ana kwa na.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa
Madam Jesca Msambatavangu

No comments:

Post a Comment