TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, March 7, 2015

Naibu Katibu Mkuu wa UDP Zanzibar amvaa Maalim Seif

index 


kuu wa UDP Zanzibar Juma Khamis Fakih amemvaa Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim
 Seif Sharif Hamad na kuigwaya kauli yake ya kuwataka wananchi kutoshiriki zoezi la upigaji wa kura ya maoni juu ya katiba inayopendekzwa .
Amesema kuwa kauli ya Katibu Mkuu wa CUF haina nia njema na wananchi wa Zanzibar na haifai kutolewa na Kiongozi wa juu wa Serikali kama huyo ambaye amepewa dhamana ya kuwaongoza na kuwatumikia wazanzibar .
Katika mahojiano maalumu na gazeti hili  Naibu Katibu huyo amewataka wananchi kuipuuza kauli hiyo na kuwahimiza kuisoma katiba inayopendekezwa ili wakati ukifika afanye maamuzi sahihi na kutumia haki yao kidemokrasia .
Amesema kuwa katiba inayopendekezwa ni suluhisho la changamoto na kero za muungano ambazo zimekuwa zikilalamikiwa kwa muda mrefu na kwamba kutoipigia kura katiba hii ni kuhalalisha kuendelea kutumika kwa katiba iliyopo ambayo ina mapungufu mengi .
“Ni vyema wananchi kuipuuza kauli ya Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar ya kuwataka kutoshiriki kura ya maoni , hii ni kauli ambayo haina nia njema na wananchi wa Zanzibar na haifai kutolewa na kiongozi wa juu wa Serikali kama yeye ”alieleza .
“Kama hatukuipigia kura katiba hii unafikiri mafuta ambayo tumekuwa tukiyadai tutayapata wapi , mikopo ya nje tutaipatawapi ? , hapa ni lazima wananchi wapime kuhusu kauli hii ” alihoji na kuongeza .
Aidha  ameongeza kwa kuwataka wananchi viongozi wa vyama vya upinzani ambao wanaoipinga katiba inayopendekezwa kuwapa uhuru wananchi wa kuamua wenyewe kulingana na maoni yao baada ya kuisoma katiba hiyo .
“Hii ni katiba ya watanzania wote na hizi kauli za viongozi akiwemo Makamo wa Kwanza wa Rais ni kama kuwalazimisha wananchi kufuata maoni yake jambo ambalo linapingana na misingi ya utawala bora ”alifahamisha .
Katika hatua nyingine Naibu Katibu Mkuu huyo amewataka wananchi wa Zanzibar hususani Kisiwani Pemba kuacha kuwa watumwa wa Kisiasa kwa kuwaepuka viongozi wanaojali maslahi yao binafsi  bali waangalie viongozi wenye nia ya kuwaletea maendeleo .
Amesema kuwa amajimbo ya Pemba ambayo vingozi wake Wabunge na Wawakilishi ambao wanatoka chama cha CUF wameshindwa kuwaletea mabadiliko ya maendeleo na badala yake wangalie viongozi walio na uwezo wa kuleta maendeleo katika majimbo yao bila ya ubaguzi .
Na Masanja Mabula –PembaNaibu Katibu M

No comments:

Post a Comment