TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, March 7, 2015

WANAWAKE CUF WETE WAWA NA MWITIKIO MDOGO WA KUGOMBEA UONGOZI

index
Na Masanja Mabula -Pemba
Mchakato wa uchukuwaji wa fomu za kugombea nafasi mbali mbali za Uongozi wa Majimbo na Wadi ndani ya Chama Cha Wananchi (CUF)  katika Wilaya ya Wete  unaendelea vyema huku kukiwa na mwitiko mdogo wa wanawake kuchukua fomu  kuwania nafasi hizo .
Ikiwa zimebakiwa siku nne (4)  kufungwa kwa zoezi hilo katika Majimbo ya Gando na Mtambwe  jumla ya wanachama kumi na tano (15) wa chama hicho wamejitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi za ubunge .
Katika nafasi ya uwakilishi jumla ya wanachama sita (6) ndiyo waliochukua fomu hizo ambapo kwa upande wa nafasi ya diwani waliochukua fomu ni wanachama sita (6) huku wadi ya Bopwe na Fundo hakuna mwanachama aliyechukua fomu .
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Katibu wa CUF Jimbo la Gando Khelef Mohammed amesema kuwa nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi ambayo inashikiliwa na Said Ali Mbarouk ni mwanachama mmoja ndiye aliyechukua fomu .
Aidha amefahamisha kwamba nafasi ya Ubunge inayoshikiliwa na Khalifa Suleiman ,  jumla ya wanachama sita wamechukua fomu ambapo katika nafasi ya diwani kwa wadi za Gando na Kizimbani amejitokeza mwananchama mmoja mmoja kila wadi .
“Hadi muda huu ni mwanachama mmoja ndiye aliyejitokeza kuchukua fomu ya uwakilishi , ambapo tumepokea wanachama sita kuwania nafasi ya Ubunge pamoja na wanachama wawili nafasi ya udiwani katika wadi za Gando na Kizimbani ” alifahamisha .
Katibu Khelef amewataja waliochukua nafasi ya Ubunge ni Khalifa Suleiman , Kassim Juma Sharif , Salim Ahmed Salim , Salim Mussa Omar , Mohamed Omar Hamad pamoja na Suleiman Salim Shukuru .
Amefahamisha kwamba nafasi ya uwakilishi aliyechukua fomu ni ALI Yussuf Abdalla na katika nafasi ya Diwani Mohammed Rashid Mohammed (Gando) na Juma Ali Salim (Kizimbani ).
Kwa upande wa Jimbo la Mtambwe kuna jumla ya wanachama tisa (9) wamechukua fomu kugombea nafasi  Ubunge , nafasi ya Uwakilishi wanachama watano (5) Diwani wanachama watano (5) akiwemo Riziki Said Juma .wadi ya Mtambwe .
Katibu wa Juma hilo Seif Said amewataja waliochukua fomu kuwania nafasi ya Ubunge ni Juma Said Omar , Said Massoud Said , Abubakar Khamis Bakar , Suleiman Ali Seif , Said Mbarouk Ali , Bakar Omar Hamad , Khalifa Mohammed Issa , Mohammed Hamad Khamis na Salim Mussa Mjaka .
Nafasi ya Uwakilishi waliochukua fomu ni Hassan Sheha Ali , Mohammed Massoud Marhuni , Habibu Ali Mohammed , Abas Ali Khamis pamoja na mwalimu Omar Ali Omar .
Aidha amezidi kufahamisha kuwa katika wadi ya Mtambwe jumla ya wanachama wannen wamechukua fomu ambao ni Mohammed Khamis Hamad , Riziki Saud Juma , Hamad Khamis Salim na Kassim Othman Kombo na katika wadi ya Kisiwani Juma Hassan Saleh amechukua fomu kutetea nafasi yake hiyo .
 
Hata hivyo amefahamisha kwamba idadi ya wanachama watakao chukua fomu inaweza kuongezeka kutokana na muda uliobaki huku pia akitoa wito kwa wanawake kujitokeza kuwania nafasi katika majimbo na kuepukana na kutegemea nafasi za uteuzi wa nafasi maalumu.

No comments:

Post a Comment