TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, March 7, 2015

MKE WA RAIS MAMA SALMA KIKWETE KUWA MGENI RASMI SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.

index
Na Happy Shirima – Habari Maelezo.
 Dar es salaam.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo [WAMA] anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yatakayofanyika Machi 8 mwaka huu katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam .
Akizungumzia maadhimisho hayo leo jijini Dar es salaam , Kaimu Mkuu wa mkoa wa Dar se salaam Mhe. Raymond Mushi amesema kuwa maadhimisho hayo mwaka huu yataongozwa na kauli mbiu isemayo “Uwezeshaji Wanawake Tekeleza, Wakati ni Sasa “.
Amesema ujumbe huo unaikumbusha jamii kujenga mazingira  wezeshi kwa kutambua mchango wa wanawake katika kuleta maendeleo ya jamii na nchi kwa ujumla .
Ameeleza  kuwa wadau kote nchini wanatakiwa kuelimishwa ili kuangali upya wajibu wao kwa kuwashirikisha, kuwaamini na kuwapa wanawake haki sawa katika nafasi za elimu , uchumi na uongozi ili waweze kuwa chachu ya maendeleo yao binafsi, familia na taifa zima.
“Lengo la maadhimisho haya ni kukumbuka wajibu wa kila mmoja  kushiriki katika mikakati  ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za wanawake kuanzia ngazi ya kaya hadi Taifa” Amesema.
Akitoa ufafanuzi kuhusu maadhimisho hayo amesema kuwa yanaambatana na maonyesho ya kazi na bidhaa mbalimbali za vikundi vya ujasiriamali na kuzishirikisha Asasi za Kiraia  zinazojishughulisha na masuala ya utoaji wa Elimu ya Uraia na sheria ya utunzaji fedha.
Ameongeza kuwa siku ya kilele  kutakuwa na maandamano yatakayoanzia Barabara ya Lumumba na kuishiaviwanja vya mnazi mmoja ambayo yatapokewa na mgeni rasmi  na wananchi  wa mkoa wa Dare s salaam.

No comments:

Post a Comment