TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, March 7, 2015

Mashabiki wamtaka Rose Muhando .Msama apata kigugumizi

indexNa Mwandishi Wetu
MASHABIKI   kadhaa  wa  muziki  wa Injili  Tanzania  wametamka kumtaka  muimbaji  nguli  wa  muziki  wa  Injili  kuwemo  katika  orodha  ya  waimbaji  watakaopanda  jukwaani  kwenye  Tamasha  la  Pasaka  linalotarajia  kufanyika  mwezi  ujao hapa nchini.
Voster  Maulid  na Kassim Mtolea wa  jijini  Mwanza  wanampenda kwa kiasi kikubwa muimbaji huyo hasa anapokuwa jukwaani.
Mashabiki  hao  walisema  muimbaji  huyo  akifanikiwa  kupanda  jukwaani anasaidia  kuteka  idadi  kubwa ya mashabiki  wanaohudhuria matamasha anayohudhuria.
Naye  Method  Millanzi  wa Mtwara  alisema Rose Muhando ni muimbaji asiye na mpinzani Tanzania, hivyo  Kamati ya maandalizi isimuache muimbaji huyo katika mchakato wa tamasha la mwaka huu.
Mkurugenzi wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema wamesikiliza kilio cha mashabiki wa muziki huo, wamelipokea suala hilo na watalifanyia kazi.
Msama  alisema  yeye  na  kamati  yake  wanaendelea  na  mchakato  wa maandalizi, watatumia  fursa  hiyo kulijadili suala hilo.

No comments:

Post a Comment