TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, January 27, 2015

WAIMBAJI WATAKA NAFASI ZAIDI TAMASHA LA PASAKA

images
Na Samia Mussa
 
WAKATI wakazi wa mikoa kadhaa hapa nchini wakiomba Tamasha la Pasaka lipite kwenye mikoa yao, baadhi ya waimbaji wakongwe wa tamasha hilo linalotimiza miaka 15 tangu kuanzishwa kwake,  wametoa mapendekezo yao kwa wandaaji Kampuni ya Msama Promotions.
Wakizungumza hivi karibuni wimbaji hao, walianza kwa kuipongeza Kampuni hiyo kufikisha miaka hiyo bila kutetereka huku wakitoa mapendekezo mbalimbali yatakayoboresha zaidi matamasha yajayo.
Moja ya mapendekezo hayo ni pamoja na kutaka kila mwimbaji apate nafasi  angalau ya kuimba nyimbo mbili ukizingatia waimbaji hao wana albamu zaidi ya tatu jambo ambalo kwao linawapa ugumu kwao pamoja na mashabiki.
Hayo alisemwa na mwimbaji nguli Upendo Nkone ambapo alisema licha ya kampuni hiyo kujitahidi kufanya vizuri ikiwa pamoja na kuimba kwa kutumia vyombo hivyo Kamati ya Maandalizi inatakiwa kubadilisha vitu vichache ikiwemo kupewa dakika za kuimba kama wanavyofanya nchi zilizoendelea si moja kama ilivyozoeleka.
“Kile ambacho naona kiwekewe mkazo tunaposema tutaimba’live  basi tufanye live kweli na mazoezi yaanze mapema wiki mbili kabla ili mwimbaji afanyie mazoezi nyimbo atakazoimba halafu tunaomba kila mwimbaji angalau aimbe nyimbo mbili, lakini utakuta unaimba nyimbo moja tu kama mimi nina albamu nne nina nyimbo nyingi ambazo watu wanazipenda unapoimba nyimbo moja, watu wanakuwa hawajatosheka kwa sababu wamelipa kiingilio,” na kuongeza.
“Idadi ya nyimbo ingozeke, wenzetu nchi nyingine wanatoa dakika 20-30 kwa kila muimbaji kwa hiyo unangalia nyimbo zenye dakika kati ya 5-7 unachanganya  kwa hiyo nusu saa unaweza ukaimba nyimbo mbili au tatu,”  alisema Nkone.
Nkone pia alitoa pendekezo kupata wajuzi wa muziki ili nyimbo hizo zipigwe kama zilivyo huku akitolea mfano kuwa yeye nyimbo zake zinatengenezwa na wenye upeo wa muziki hivyo lazima zipigwe vile ninavyotengenezewa kwenye CD yake, kwenye ‘live’ kuna vitu vinapungua hivyo awawekee wajuzi wa hali ya juu.
Alisema kuwa sababu nyingine itakayofanikisha maendeleo zaidi katika Tamasha hilo la 15 itafanya Msama Promotions iwe katika kiwango cha juu kwa sababu inabeba waimbaji vingunge waimbaji wazito ni kuanza mazoezi mapema na kwa taratibu zilizopangwa, kupatiwa ratiba ya kila muimbaji ajitambue cha kufanya kabla ya kupanda jukwaani.
Upendo Kilahiro  anaipongeza Msama kwa kutimiza 15 tangu imeanza kuandaa tamasha hilo kubwa hapa nchini, huku akiiomba kampuni hiyo kubwa kumiliki vyombo vyake ambavyo vitatumika katika matamasha yake.
“Naomba Mungu Msama ingepata vyombo vyake kwa sababu  ni kampuni ya muda mrefu na muda huu wote tunakodisha, ingepata vyombo katika ule ubora wake tunaohitaji tukivimiliki wenyewe tutajua muda gani tutavifunga na injinia wenu atakaa sawa avirekebishe  kwa hiyo hadi tamasha linanza hakuna ucheleweshaji”.
“Kwa sababu vifaa vitakuwa vimekaa vizuri na kwa kuwa ni vyenu mnakuwa mnavijua na mtakuwa mnajua udhaifu mmepiga hatua kubwa, miaka 15  mmeweza kumiliki vyombo vyenu ambavyo vikafaa uwanja wa wazi na ndani itakuwa ni hatua moja na tutawakilisha vizuri kazi zetu  mara nyingi sauti zimekuwa zikituchelewesha kuanza,” alisema Kilahiro.
Mwimbaji huyo alisema kuwa endapo vyombo vitapatikana Saundi ikiwa nzuri mwimbaji yeyote atafurahi na kazi yake itaonekana na hata watu watafurahi.

No comments:

Post a Comment