TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, January 27, 2015

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

index16
Mtu mmoja mkazi wa kitongoji cha chang’ombe auawa kwa kupigwa na wananchi.
Mtu mmoja mkazi wa kijiji cha mkutano wilayani momba auawa na kisha mwili wake kutupwa shambani.mtu mmoja mkazi wa ilomba jijini mbeya afariki dunia papo hapo baada ya kugongwa na semi traller.
KATIKA TUKIO LA KWANZA
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la mwinzala sekele mwenye umri kati ya miaka 40 – 45 Mkazi wa kitongoji cha chang’ombe – mshewe aliuawa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kundi la wananchi walioamua kujichukulia sheria mkononi.
mwili wa marehemu ulikutwa umetelekezwa mnamo tarehe 26.01.2015 majira ya saa 11:00 Asubuhi huko katika kijiji na kata ya mshewe, tarafa ya bonde la usongwe, wilaya ya kipolisi mbalizi,
                Inadaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni kulipiza kisasi kufuatia marehemu kutuhumiwa Kuhusika katika tukio la mauaji ya sekela kaini mkazi wa kijiji cha mshewe ambaye alikutwa ameuawa na kutupwa katika shamba la mahindi kijijini hapo tarehe 24.01.2015 majira ya saa 15:45 alasiri.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna msaidizi wa polisi barakael n. masaki anatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za mahali walipo watuhumiwa waliohusika katika tukio hili Azitoe katika mamlaka husika kwa hatua zaidi za kisheria wakati uchunguzi na upelelezi zaidi wa tukio hili unaendelea.
KATIKA TUKIO LA PILI:
Mtu mmoja mkazi wa kijiji cha mkutano wilayni momba aliyetambulika kwa jina la hamis Simwawa (25) alikutwa ameuawa shambani kwa kukatwa shoka shingoni na kisha kunyofolewa viungo vya mwili ambavyo ni ulimi, meno ya chini na jicho la kushoto.mwili wa marehemu ulikutwa shambani mnamo tarehe 26.01.2015 majira ya saa 08:00 asubuhi Huko katika kijiji cha mkutano, kata ya nzoka, tarafa ya ndalambo, wilaya ya momba, mkoa wa mbeya. inadaiwa kuwa kabla ya watu hao kufanya tukio hilo walimwita marehemu ili awasaidie kazi za shambani na kisha kumuua. inadaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni imani za kishirikina. watuhumiwa wawili wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo ambao ni 1. kawawa sinkala (31) na 2. emanuel sinkala (15) wote wakazi wa kijiji cha mkutano.
KATIKA TUKIO LA TATU:
Mtu mmoja mkazi wa ilomba jijini mbeya aliyefahamika kwa jina la joshua andendekisye Mwaisanila (35) alifariki dunia baada ya kugongwa na gari lenye namba za usajili t.189 blk/t.193 blk Aina ya semi traller lililokuwa likiendeshwa na dereva aitwaye ahazi cheyo (24) mkazi wa iyunga jijini mbeya.
Aukio hilo limetokea mnamo tarehe 26.01.2015 majira ya saa 09:05 asubuhi huko forest katika Barabara ya mbeya/tunduma. chanzo cha ajali kinachunguzwa. dereva amekamatwa. mwili wa marehemu umehifadhiwa.
HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna msaidizi wa polisi barakael n. masaki Anatoa wito kwa madereva kuwa makini wanapotumia vyombo vya moto ikiwa ni pamoja na kuzingatia sheria na alama za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoepukika.
imeasainiwa na:
[barakael n. masaki – acp] kaimu kamanda wa polisi mkoa wa mbeya.

No comments:

Post a Comment