TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, January 26, 2015

PROFESA SOSPETER MUHONGO WAKATI WA KUBWAGA MANYANGA

DSCF1880
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akizungumza na waandishi wa katika mkutano uliofanyika mchana huu kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za Wizara hiyo,zilizopo kwenye Mtaa wa Samora,Jijini Dar es salaam.
Waziri Muhongo ametangaza kujiuzulu wadhifa wake huo,kufuatia shinikizo la muda mrefu la kumtaka afanye hivyo au awajibishwe, kufuatia mapendekezo ya Bunge lililopita, lililoagiza serikali kuchukua hatua dhidi yake na wengine kadhaa kufuatia kashfa ya akaunti ya Tegeta Escrow. Kwa hisani ya http://issamichuzi.blogspot.com/ DSCF1860Waziri Muhongo akikazia kujiuzulu kwake huko amesema kuwa yeye sio mla rushwa bali ni mchapa kazi tu na akilizungumzia swala la akaunti ya Tegeta Escrow ambalo ndilo lililopelekea kujiuzulu kwake huko,Waziri Muhongo amesema kuwa sakata hilo lilitawaliwa na mambo makuu manne ambayo aliyataja kuwa ni Mvutano wa kibiashara, Mvutano wa kisiasa, Mvutano wa uongozi na madaraka pamoja na Ubinafsi.
Hivyo kasema ameamua kujiuzulu ili kuiachia Serikali na Bunge kusitisha malumbano ya sakata la Escrow, akidai inaonekana yeye ndiyo tatizo.Picha/habari na Othman Michuzi. DSCF1873Sehemu ya Waandishi wa kutoka vyombo mbali mbali vya habari wakifatilia kwa makini taarifa ya Waziri Muhongo.

No comments:

Post a Comment