Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa nne kutoka kushoto akipokelewa
kwa mchakamchaka na Mbunge wa jimbo la Donge na Mwenyekiti wa UVCCM
Taifa Ndugu Sadifa Juma Khamis wa tatu kutoka kushoto pamoja na vijana
wa jimbo hilo ambao walikimbia naye umbali wa kilomita moja wakiwa
katika mapokezi hayo yaliyotia fora mara baada ya kuanza ziara yake
katika jimbo hilo mwishoni mwa juma akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi
na Uenezi CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana yuko katika ziara ya visiwa vya
Unguja na Pemba Zanzibar akihimiza uhai wa Chama cha Mapinduzi na
kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa sambamba na Nape Nnauye katika mchakamchaka wakati wa mapokezi hayo katika jimbo la Donge Kaskazini Unguja.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katikati,
Mbunge wa jimbo la Dole Sadifa Juma Khamis wakikabidhi mifuko ya saruji
kwa Bakari Ame Hussein mwalimu mkuu wa skuli ya msingi ya Mahonda jimbo
la Donge.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wanafunzi wa Skuli ya Awali Mahonda jimbo la Donge.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifurahia
jambo wakati Salum Gharib Salum Mwenyekiti wa kamati ya Skuli ya
Sekondari ya Bumbwini Misufini jimbo la Dole mara baada ya kupokea
mifuko 50 ya saruji kutoka kwa mbunge wao Sadifa Juma Khamis na Mabati
200 kutoka kwa Katibu Mkuu Abulrahman Kinana
Salum Gharib Salum Mwenyekiti wa kamati ya Skuli ya Sekondari ya Bumbwini Misufini jimbo la Dole
akishukuru mara baada ya kupokea misaada hiyo ya vifaa vya ujenzi
kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na mbunge Sadifa
Juma Khamis.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na mbunge Sadifa Juma Khamis wakishiriki ujenzi wa skuli ya Bumbwini Misufini.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye wakikagua skuli ya skuli ya Mahonda.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akizungumza jambo mara
baada ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushiriki ujezni
wa ofisi ya CCM tawi la Muembe Jogoo.
Baadhi
ya wanafunzi wa madarasa ya Amali huko Kinduni jimbo la Kitope
wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM wakati alipokagua na kujionea shughuli
mbalimbali wanazofanya katika masomo yao .
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi majiko ya genzi ya
kupikia kwa wanafunzi vijana wa madarasa ya Amali huko Kinduni jimbo la
Kitope
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakiangalia shughuli mbalimbali za vijana wa mafunzo ya Amali katika mambo ya mapishi..
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakiangalia shughuli mbalimbali
za vijana wa mafunzo ya Amali katika mambo ya ushonaji wa nguo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
akishiriki kazi za ushonaji huku Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
akiangalia shughuli mbalimbali za vijana wa mafunzo ya Amali katika
mambo ya ushonaji wa nguo.
Kikundi cha Ngoma kikitumbuiza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Maskani ya CCM Kizota jombo la Kitope.
Mbunge wa jimbo la Donge na Mwenyekiti wa UVCCM Ndugu Sadifa Juma Khamis akiwahutubia wananchi katika mkutano huo.
Balozi Ali Karume akitema cheche zake kuhusu Katiba Mpya iliyopendekezwa na kuwashawishi wananchi waipigia kura ya ndiyo.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo.
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiwahutubia wananchi katika mkutano huo uliofanyika Maskani ya CCM Kizota.
Makamu wa Pili wa Rais wa Rais wa Zanzibar Mh. Balozi Seif Ali Idd akiwahutubia wananchi wa jimbo la Kitope Kaskazini Unguja.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika
mkutano huo na kuwsiki waipigie kura ya ndiyo katiba inayopendekezwa kwa
kuwa ina mambo mengi yenye faida kwa wazanzibari.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiagana na
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd mara baada ya
mkutano huo kumalizika, Kushoto anayefurahia ni Nape Nnauye Katibu wa
NEC Itikadi na Uenezi.
No comments:
Post a Comment