TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, February 1, 2015

MAMA NA MTOTO MPANGO WA SERIKALI KUPUNGUZA VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI

3 Na Lorietha Laurence- Maelezo Dodoma
Serikali imeandaa mikakati mbalimbali ya kuboresha afya ya wanawake wajawazito ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi. Akijibu swali kwa Niaba ya Waziri wa Afya na Ustawi, katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni mjini Dodoma, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Dkt. Pindi Chana amesema moja ya mikakati hiyo ni mpango mkakati ulioboreshwa wa kuendeleza kasi ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi uliozinduliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete mwaka 2014. Alisema kuwa mpango huo unawashirikisha wadau mbalimbali ambao ni World Lung Foundation, Plan International, Care International, Jhpiego, UNFPA na GIZ wanaochangia katika kupanua vituo vya afya ,kujenga vyumba vya upasuaji na ununuzi wa vifaa na tiba. “Mkakati huu ni jitihada za serikali katika kuhakikisha afya ya mama na mtoto inaboreshwa kwa kukomesha vifo vitokanavyo na uzazi na watoto walio chini ya umri wa miaka mitano” alisema Dkt. Chana. Alifafanua kuwa Rais Dkt Kikwete ameagiza wakuu wa mikoa kusimamia masuala ya afya kwa ngazi zote zinahusu afya ya mama na mtoto na kuhakikisha wanawasilisha taarifa za maendeleo ya utekelezaji kila baada ya miezi mitatu(3). Mpango mkakati huo umeanzishwa kutokana na bajeti finyu ya afya ya mama na mtoto ambayo imekuwa ikipungua kila mwaka wa fedha , hivyo serikali ikaona umuhimu wa kuangalia njia mbadala ya kuweze kupata fedha ili kuongeza bajeti.

No comments:

Post a Comment