TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, February 5, 2015

Jumuiya ya Afrika Mashariki mfano wa kuigwa Afrika- Rais Gauck

images Immaculate Makilika –MAELEZO ARUSHA
Rais wa shirikisho la Ujerumani,Jochim Gauck ameonesha  kufurahishwa  na utendaji wa kazi wa Jumuiya ya afrika mashariki, EAC,  na kusema  ikiwa Jumuiya hii itatimiza malengo yake iliyojiwekea basi itakua mfano bora Afrika’.
 
Rais huyo ameyasema hayo leo alipotembelea makao makuu ya jumuia ya Afrika Mashariki EAC, mjini Arusha, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku sita nchini na kusema kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC inafaida ya kuwa na nchi zenye uchumi unaendelea kukua kwa asilimia 6 katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.
 
Amesema kuwa  Jumuia ya Afrika Mashariki ina watu zaidi ya milioni 145 huku wengi wao  wanazungumza lugha moja ya kiswahili pamoja na kuwa na tamaduni tofauti, na kuongeza kuwa Jumuiya ya nchi za Ulaya EU hawana neema ya namna hii.
 
Rais Gauck ameelezea uhusiano mzuri uliopo baina ya Shirikisho la Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC na Shirikisho la Jumuiya ya Nchi za Ulaya EU na kusema kuwa zinafanana kwa kiasi kikubwa hasa katika masuala ya utengamano wa kisiasa.
 
Hivyo jumuiya hizo hazina budi kushirikiana pamoja katika masuala mbalimbali yenye kuleta tija. 
 
‘Msiwaamini wanaosema Shirikisho la Jumuiya ya Nchi za Ulaya limekufa’ alisema Rais huyo, na kuongeza pia si kweli kwani hivi sasa Jumuiya hiyo ipo na imeendelea kuwa na nguvu kuliko ilivyokuwa mwanzo, isipokuwa imekabiliana na changamoto zake alisema.
 
Kwa upande wake Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Harrison Mwakyembe ameeleza kuwa, Tanzania ni Mshiriki wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na ujio huu ni muhimu kwa kuwa Ujerumani inauzoefu katika
Masuala haya ya mtengamano.
 
Amesema, Ujerumani imekua msaada mkubwa sana kwa Jumuiya hii tangu ianzishwe hadi sasa imetoa jumla ya Euro milioni 100. Waziri Mwakyembe ameendelea kwa kusema tuwe na imani na kuijengea Jumuiya umoja, kwani tukiungana tutapata faida kubwa kuliko kutengana.
 
Aidha, Mbunge wa Bunge la Shirikisho la Afrika Mashariki Mhe. Jesca Erio ameshukuru ujio wa kiongozi huyo na kuahidi kuendeleleza uhusiano mzuri kati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Serikali ya shirikisho la Ujerumani na Taasisi zake kama GIZ pamoja na mashirika yanayojishughulisha na masuala ya haki za binadamu.Baada ya wiki mbili Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  anatarajia kuwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya.

No comments:

Post a Comment