TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, February 4, 2015

Wamiliki wa shule za sekondari watakiwa kuzingatia viwango vya ufaulu

kilango
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Anna Kilango Malecela akijibu swali la Mh. Joseph Selasini Mbunge wa Rombo.
selasini
Mbunge la Mbunge wa Rombo Joseph Selasini, akiuliza swali.

………………………………………………………………………….
Na Lorietha Laurence-Maelezo,Dodoma Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Anna Kilango Malecela ametoa wito kwa wamiliki wote wa shule binafsi pamoja na za serikali kuzingatia kiwango cha ufaulu kutoka kidato kimoja kwenda kingine kilichowekwa na serikali. Akijibu swali la Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini, bungeni mjini Dodoma aliyetaka kujua kama Serikali inajua na kuunga mkono kiwango cha ufaulu kwa shule zisizo za Serikali zinazoweka viwango maalum vya ufaulu tofauti na vile ilivyoviweka. Naibu Waziri Anne Kilango alisenma Serikali haiungi mkono utaratibu huo kwa kuwa umekiuka waraka wa elimu namba 12 wa mwaka 2011 na waraka Namba 4 wa mwaka 2012. “Napenda kusisitiza kuwa yeyote atakayekaidi maelekezo haya ya serikali atachukuliwa hatua kali za kinidhamu kwa mujibu wa sheria ya elimu Namba 25 sura ya 353 kifungu cha 35” alisema Kilango Aliongeza kuwa Waraka wa Elimu Na. 6 wa mwaka 2011 umetoa maelekezo kuhusu wastani wa ufaulu katika mtihani wa Kitaifa wa kidato cha pili ambao ni asilimia 30. Hivyo aliwataka walimu waelewe kuwa wanafunzi wanatofautiana katika uelewa hivyo kuweka kiwango kikubwa cha wastani kunasababisha wanafunzi kukosa fursa ya kuendelea na masoma na hivyo kuanza utaratibu mpya ya kutafuta shule. Alibainisha kuwa Serikali itazindua program ya KKK Februari 7, 2015 ikiwa na nia madhubuti ya kuboresha elimu kwa shule zote za serikali katika kutoa elimu bora kwa wananchi .

No comments:

Post a Comment