TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, February 6, 2015

Ujerumani iko tayari kushirikiana na mahakama ya Afrika

index
Immaculate Makilika –MAELEZO ARUSHA
Rais wa  Shirikisho la  Ujerumani amesema Serikali yake iko tayari kushirikiana na Mahakama ya Afrika katika utendaji kazi wake ili kusaidia  kutoa huduma iliyokusudiwa kwa walengwa.
 
Rais huyo ameyasema hayo leo alipotembelea Mahakama ya  Afrika iliyopo  mjini Arusha, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku sita nchini na kusema kuwa angependa kuona utawala wa  sheria ambao unaozingatia demokrasia  unafuatwa na kuheshimiwa.
 Aidha, Rais Ghauck ameipongeza mahakama hiyo kwa weledi wake na hatua nzuri waliyofikia huku akitolea mfano kesi iliyosikilizwa mwaka 2014 huko Adis Ababa, Sudan.
‘Tunaunga mkono maendeleo pia  tungependa kuendelea kushirikiana nanyi, msisite kutuomba msaada  alisema Rais Gauck’.
 
Naye kwa upande wake Jaji Mkuu wa Mahakama ya Afrika Augustino Ramadhani  alisema Serikali ya Ujerumani imekua na ushirikaiano mzuri na Mahakama hiyo kwani ilisaidia pia katika ujenzi wake.
 
Hata hivyo jaji Ramadhani amesema wamemuomba Rais wa Ujerumani asaidie kujenga mahakama ya Afrika ya Mashariki, ombi ambalo Rais huyo amesema atalishughulikia kushirikiana na  viongozi aliongozana nao.
 
Aidha, Jaji Ramadhani amesema kuwa uwepo wa Mahakama hii Afrika ni jambo la kujivunia  kwani itaweza kusaidia matatizo ya waafrika wote kutoka sehemu  mbalimbali.

No comments:

Post a Comment