TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, February 6, 2015

Benki ya Exim yaadhimisha Siku ya Saratani Duniani na Watoto wenye Saratani Hospitali ya Taifa Muhimbili

exim1Mkuu wa matawi wa Benki ya Exim, Bi. Elizabeth Mayengoh, akikabidhi vitabu kwa mmoja wa watoto waliolazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwenye wodi maalum ya watoto wanaougua ugonjwa wa saratani katika kuadhimisha siku ya saratani duniani. Wanaoshudia ni baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Exim na wazazi wa watoto hao. Benki hiyo ilikabidhi vifaa mbalimbali vikiwemo vyakula, vifaa vya kuchezea, sabuni, vifaa vya shule nk, lengo likiwa ni kujenga uelewa kuhusiana na ugonjwa wa saratani mpango unaoendana na kauli mbiu ya mwaka huu ya Siku ya Saratani Duniani inayosema kuwa tatizo la saratani “lipo ndani ya uwezo wetu”.
exim2Meneja masoko msaidizi wa Benki ya Exim, Bi. Anita Goshashy akishikana mikono na Dr. Livin Mumbari  Daktari wa watoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, muda mfupi baada ya benki hiyo kukabidhi vifaa mbalimbali kwa watoto waliolazwa hospitalini hapo kwenye wodi maalum ya watoto wanaougua ugonjwa wa saratani katika kuadhimisha siku ya saratani duniani. Wanaoshudia ni baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Exim na wazazi wa watoto hao. Benki hiyo ilikabidhi vifaa mbalimbali vikiwemo vyakula, vifaa vya kuchezea, sabuni, vifaa vya shule nk, lengo likiwa ni kujenga uelewa kuhusiana na ugonjwa wa saratani mpango unaoendana na kauli mbiu ya mwaka huu ya Siku ya Saratani Duniani inayosema kuwa tatizo la saratani “lipo ndani ya uwezo wetu”.

No comments:

Post a Comment