TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, February 2, 2015

RAIS WA UJERUMANI KUWASILI LEO USIKU , MAANDALIZI YA MAPOKEZI YAKE YAKAMILIKA.

Na. Aron Msigwa –MAELEZO.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Said Meck Sadiki amewaomba wakazi wa jiji la Dar es salaam kujitokeza kwa wingi katika mapokezi ya Rais wa Shirikisho la Ujerumani Mh.Joachim Gauck  anayetarajiwa kuwasili nchini Tanzania leo usiku kwa ziara ya kikazi ya siku tano.

Akizungumzia ujio wa rais huyo ofisini kwake  leo jijini Dar es salaam Mh. Meck Sadiki amesema kuwa rais Joachim Gauck na msafara wake atawasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere majira ya saa 2.30 usiku na kulakiwa na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete.

Ameeleza kuwa mapokezi rasmi ya rais huyo yatafanyika kesho katika viwanja vya Ikulu majira ya saa 3 asubuhi ambapo rais huyo akiwa na mwenyeji wake atapata fursa ya kukagua gwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili yake na Jeshi la Wananchi wa Tanzania na kupigiwa mizinga 21.

Amesema kuwa akiwa nchini Tanzania Rais Joachim Gauck atakuwa na mazungumzo ya faragha na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu jijini Dar es salaam na baadaye kufanya mazungumzo na baadhi ya viongozi wa Vyama vya hiari, uongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani pamoja na kukutana na wafanyabiashara wa Dar es salaam.

Amefafanua kuwa Februari 4, 2015, Rais huyo ataelekea Zanzibar ambapo atakutana na kuwa na mazungumzo na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na viongozi wengine wa Serikali.

Aidha kabla ya kuhitimisha ziara yake nchini Tanzania  Februari 6, 2015 rais huyo wa Shirikisho la Ujerumani atatembelea mbuga ya wanyama ya Serengeti ,Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki  na Mahakama ya Kimataifa ya Haki za Binadamu jijini Arusha.

No comments:

Post a Comment