TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, February 4, 2015

Serikali ya Tanzania yapokea takribani shillingi bilioni 15.5 kutoka Uganda

malima
Naibu Waziri wa Fedha  Adam Malima.
………………………………………………………………………………………….
Na Lorietha Laurence-Maelezo Dodoma
Serikali ya Tanzania imepokea takribani shillingi bilioni 15.5 kutoka Serikali ya Uganda ikiwa ni fidia itokanayo na athari za vita vya Kagera.
Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima ameeleza hayo Bunge mjini Dodoma kuwa fidia iliyokuwa inatakiwa kulipwa ni Dola za Marekani milioni 18.4 ingawa Uganda imelipa Dola milioni 9.7 zilizoingizwa kwenye mfuko mkuu wa Hazina.
“Kiasi hicho cha fedha kilipokelewa na kuwekwa katika Mfuko Mkuu wa Hazina kwa ajili ya matumizi ya maendelao ya wananchi ” alisema Malima.
Alibainisha kuwa taratibu za fidia zitokanazo na hasara za vita hiyo zinaongozwa na sheria na kanuni za kimataifa pamoja na utaratibu wa kutathmini kiwango cha hasara kitokanacho na vita.
Aliongeza kuwa licha ya kwamba vita hivyo viliathiri taifa zima la Tanzania ,mkoa wa Kagera umepokea fedha kutoka Mfuko Mkuu wa serikali ambayo imesaidia kusukuma maendelao ya wananchi.

No comments:

Post a Comment