TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, February 2, 2015

Wateja wa Airtel kushinda gari Moja Kila Siku Kupitia huduma ya Airtel Yatosha

Airtel Tanzania leo imezindua promosheni  kabambe ijulikanayo kama Airtel Yatosha Zaidi kwa wateja wanaotumia vifurushi vya Airtel Yatosha kuweza kujishindia gari Aina ya Toyota IST kila siku
Akiongea wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo Mkurugenzi wa Masoko ya Airtel Bwana Levi Nyakundi alisema” promosheni hii ni nafasi ya peeke wa wateja wetu wanaojiunga na vifurshi vya Airtel yatosha vya siku, wiki na mwezi kupata faida zaidi kutokana pesa wanazozitumia.
 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano, (kulia) akifafanua jambo wakati wa Uzinduzi huo, kushoto ni Mkuu wa Masoko,Levi Nyakundi,  
 Hii ni promosheni ya aina yake ambapo wateja wetu wanazawadiwa kutokana na matumizi yao ya kawaida ya vifurushi vya Yatosha.  tunatoa wito kwa wale ambao hawajajiunga na vifurushi vya Airtel yatosha kufanya hivi na kupata nafasi ya kushinda gari moja kila siku”aliongeza  Mallya


Baadhi ya waandishi wa Habri wakiwa Kwenye Hafla hiyo Leo
 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano, (kulia) akifafanua jambo wakati wa Uzinduzi huo, kushoto ni Mkuu wa Masoko,Levi Nyakundi,
Wapiga Picha wa Vyombo mbali mbali vya habari wakiwa kwenye Hafla hiyo ya Uzinduzi Mapema Leo iliyofanyika kwenye Eneo la wazi la Mliman City.


·        Promosheni ya Airtel yatosha zaidi itawawezesha wateja wa Airtel kushinda Toyota IST moja Kila siku
 Nia yetu  kuhakikisha tunatoa huduma na bidhaa bora kwa kupitia huduma yetu ya Airtel Yatosha huku tukiwazawadia wateja wetu zawadi nono.
Tunaamini promosheni hii itawapatia wateja wetu uzoefu tofauti wakati wote wakitumia huduma zetu za Airtel Yatosha. Zaidi ya wateja wetu kijishindia magari promosheni hii ya Airtel Yatosha Zaidi itawapatia wateja wetu vifurushi zaidi “Aliongeza Nyakundi
Akiongea kuhusu namna ya kushiriki Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya alisema” ili kushiriki kwenye promosheni hii wateja wanatakiwa kuendelea kununua vifurushi vyao vya Yatosha vya siku, wiki na mwenzi.  hakuna gharama ya ziada, kwa kununua vifurushi vya yatosha tayari utakuwa umeunganishwa kwenye droo ya yatosha zaidi na kupata nafasi ya kujishinidia Toyota IST moja kila siku
 
Kununua vifurushi vya yatosha wateja wanaweza au  kupiga *149*99#, kunua kwa kupitia huduma ya Airtel Money au kwa kununua vocha ya Airtel yatosha inayopatikana katika maduka yetu nchi nzima 
 
Mwaka Jana Airtel ilizindua huduma ya kisasa ya kibunifu na yenye vifurushi vya gharama nafuu sokoni. Kuzinduliwa kwa promosheni hii ya Airtel yatosha Zaidi ni mwendelezo wa dhamira ya Airtel ya kutoa huduma bora huku ikiwazawadia wateja wake kwa kutumia huduma zake
Mwisho

No comments:

Post a Comment