Tunaukaribisha mwaka 2013 kwa kuwaletea ubao mpya wa malumbano ya hoja:
Filosofa Forum (www.filisofaforum.com)
Katika fani hii ya mawasiliano, 
iwe kwa blog za jamii, barua pepe, magazeti, tovuti na aina nyingine 
nyingi, jambo moja ambalo baadhi yetu wadau wa malumbano ya hoja 
tungependa kuweka juhudi kulibadilisha katika mwaka huu mpya 2013, ni 
jukwaa la habari, mipasho (malumbano) ya kisiasa, kimichezo, na utani wa
 kikabila, wenye ustaarabu na maadili yaliyopevuka bila kudhihaki 
jinsia, dini, maumbile au kabila la mtanzania yeyote. Awe mtoto, kijana,
 mzee, mvulana, msichana, mwanaume au mwanamke, Filosofa Forum inaamini 
sisi sote ni matokeo ya uumbaji wa mwenyezi mungu.
Hivyo basi  kama unaamini kwa 
dhati kuwa huu ndo mwelekeo unaostahili katika malumbano ya hoja bila 
vioja, hapa ndio mahali muafaka ambapo mijadala ya aina zote itazingatia
 maadili , uwazi, na kuheshimu tofauti za kiitikadi, dini , na tamaduni 
zote za mtanzania.
KARIBUNI SANA UELIMIKE NA KUELIMISHA WENGINE
Happy New Year 2013
By Filosofa Forum team.
No comments:
Post a Comment