Chama
 cha Ngumi za Kulipwa Cha Afrika ya Mashariki na Kati (ECAPBA) kimepata 
nyumbani baada ya Mstahiki Meya wa jiji la Arusha  Mh. Gaudence Lyimo 
kuomba kihamie Arusha ili kiweze kukaa karibu na “Jumuiya ya Afrika ya 
Mashariki, EAC”Rais
 wa ECAPBA Onesmo Ngowi alimhakikishia mstahiki meya kuwa ECAPBA 
itahamishia makao yake makuu katika jiji la Arusha. Kwa sasa ECAPBA ina 
makao yake makuu katika Halmashauri ya Manispaa ya Moshi.
 Juhudi
 za Mstahiki Meya Gaudence Lyimo za kukuza michezo na kukuza utalii 
katika jiji la Arusha ni moja ya sababu zilizomfanya rais wa ECAPBA 
kuamua kuhamishia makao makuu katika jiji la Arusha.
 Uamuzi
 huo uliungwa mkono na mmoja wa wanachama wa  ECAPBA bw. Daudi Chikwanje
 ambaye ndiye Katibu Mkuu wa Chama Cha Ngumi za Kulipwa Cha Malawi!
 Nchi
 ya Malawi ni mwanachama wa ECAPBA pamoja na Kenya, Zambia, Ethiopia, 
Burundi, Sudan ya Kusini, DRC, Rwanda, Uganda na Sudan.
 ECAPBA inaratibu ubingwa unaojulikana kama ECAPBF ambao unawapa mabondia wa ukanda huu kuwa mabingwa imara wa ngumi Afrika.

No comments:
Post a Comment