Mkurgenzi
 wa Tanpress Mobini Sarya akiwa kwenye usafiri wa pikipiki akitoka 
kwenye visiwa vya Nyamango na Chembaya eneo la Mwalo wa Kanyara ziwa 
Victoria mkoani Mwanza ambako alikwenda kuchunguza upatikanaji wa  
huduma za afya katika visiwa hivyo  Novemba mwaka huu. 
Hii ndiyo ofisi ya kijiji cha Lushamba inayohudumia visiwa saba vyenye wakazi elfu 25 .
Hii
 ndiyo ofisi ya kitongoji cha Kanyara kwa juu kama inavyoonekana kwa 
chini ni Sero (Mahabusu)inayotumika kuwahifadhi wa halifu ambayo 
mwandishi wa habari  Mobini Sarya aliwekwa chini ya ulinzi kwa masaa 6.
Wakazi wa kisiwa cha  Nyamango na Soswa wakigombania usafiri wa boti kwa ajili ya kuelekea Sengerema mkoani Mwanza.
……………………………………………………………
Nyamango/Soswa visiwa vyenye fursa tele za uwekezaji
zinahitajika zahanati,shule na kumbi za starehe.
Na Tanpress,Nyamango
NYAMANGO na Chembaya ni visiwa 
viliopo maili 46 Mgharibi mwa jijini Mwanza ingawa vinahesabiwa kuwa 
vipo wilayani Sengerema  Mkoa wa Mwanza.
Hivi visiwa vina undwa na 
vitongoji viwili vyenye visiwa vinne vikijulikana kwa majina ya 
kitongoji cha Nyamango/Chamagati na Chembaya/soswa vikiwa maeneo ya 
karibu. 
Vinakisiwa kuwa na wakazi zaidi ya
 10,000 ambao wanategemea shughuli za uvuvi wa dagaa na samaki 
wanaopatikana katika ziwa viktoria.
Usafiri unaotumika kwenda kwenye 
visiwa hivyo ni boti au meli za watu binafsi,ambazo hutumia  masaa 12 
kutoka jijini mwanza eneo hilo na mara nyingi boti ya mwendo kasi 
huingia saa mbili usiku.
Aidha kutoka katika visiwa hivi 
hadi kwenye mwalo wa Kanyara ambayo ni nchi kavu ya wilaya ya Sengerema 
boti hutumia masaa manne hadi masaa matatu kufika nchi kavu.
Pia kutoka eneo la kitongoji cha Kanyara usafiri ni wa shida Km.80 hadi kufika Sengerema mjini zilipo huduma zote za kijamii.  
Eneo hilo lina vitongoji viwili 
vinavyoundwa na visiwa vine ambavyo ni Soswa/Chembaya na 
Nyamango/Chamagati ni katika eneo hilo lenye makazi ya kudumu ya watu 
ndipo frusa za uwekezaji zipojitokeza.
Hivi karibuni Mwandishi wa Shirika
 la habari Tanpress alifika kwenye visiwa hivyo kwa lengo la kukusanya 
habari na matukio ndipo alipojionea frusa nyingi za uwekezaji.
Kwanza licha ya kwamba wavuvi 
wengi ni watu wanaopenda starehe hasa za ulevi lakini ‘viwanja 
vyakujirusha’kuburudika ni kama havitoshi.
Maeneo mbalimbali ambayo mwandishi
 wa Tanpress alitembelea alikuta wenyeji wakipata vinywaji kwenye baa 
zinazofanana na vilabu vya Pombe za kienyeji jambo linaloonyesha kuwa 
maeneo hayo yanahitajika uwekezaji wa baa na mahoteli ya kisasa.
Aidha nishati ya umeme kwenye eneo
 hilo inahitajika kwa haraka kwani wengi wanatumia jeneretor ambazo 
hawamudu kununua mafuta hivyo hata wale wachache waliojitolea kujenga 
nyumba za kulala wageni wanawasha vibatari wasijue la kufanya.
Hivyo anahitajika ,mwekezaji 
mkubwa aweke mashine inayotumia mafuta ya diseli kwa ajili ya kuzalisha 
umeme wa kutosha katika eneo hilo,ambalo kwasasa lipo gizani ingawa 
wenyeji wanahitaji huduma hiyo.
Pia sio lazima itumike mashine ya 
mafuta pia hata umeme wa jua au kufuka mitambo ya upepo kwasababu maeneo
 yale hakuna miti ya kuzuia upepo huo.
Baadhi ya maeneo ,mengine au hata 
visiwa vingine  mashine za kufua umeme kwa kutumia mafuta ya diseli ndio
 zinatumika kusambaza umeme jambo ambalo halijafanyika kwenye visiwa vya
 Nyamango.
Frusa nyingine uwekeza ambayo 
inalipa  ni kituo cha afya au zahanati,licha ya kwamba wavuvi 
wanafamilia zinazohitaji huduma ya afya wanapo ugua au akinamama 
wanapotaka kujifungua huduma hiyo haipo kabisa kwenye visiwa hivyo.
Kwa hiyo akitokea mwekezaji 
akafungua zahanati yenye uwezo wa kuzalisha akinamama wajawazito anaweza
 akanufaika kwa haraka kwasababu inavyoonekana serikali imeamua 
kutelekeza wakazi hao na haina mpango wowote wa kuwajengea zahanati.
Kwasasa zahanati sio jambo la 
mjadala inahitajika kwa haraka kuweza kuokoa maisha ya akinamama 
wajawazito na watu wa kawaida wanao umia kwenye starehe zikiwemo ulevi.
Ni vyema kama mwekezaji anavutiwa 
na uwekezaji huo akajenga kabisa kituo kikubwa cha afya kwasababu hakuna
 kituo karibu hata kwenye visiwa vya jirani kama zilagula na Yozwa bado 
huduma hiyo wana kwenda kuitafuta mbali.
Elimu ni frusa nyingine ya 
uwekezaji inayohitaji watu wenye mitaji kwani pamoja na kwamba wavuvi 
hao wanafamilia zao eneo hilo lakini kuna shule moja ya umma ambayo hata
 hivyo haitoshi mahitaji.
Shule hiyo ya msingi inajulikana 
kama Soswa shule ya Msingi bado haijaweza kutoa elimu bora kutokana na 
kukosekana kwa walimu wa kutosha eneo la visiwa hivyo.
Kwa hiyo zinahitajika shule za 
awali kwa kila kisiwa ambapo  kuna visiwa vinne pia zinatakiwa  shule 
binafsi za sekondari na msingi au hata vyuo vya michezo ya majini kwa 
ajili ya wagoeleaji.
Frusa zingine niliziona ni kuweka 
boti za mwendo kasi kwa ajili ya kuwakimbiza wagonjwa hospitalini na 
kuanzisha kampuni za ulinzi kwani hivi sasa baada ya uvamizi kuwepo, 
wakazi wa pale wameanza kukodi walinzi kutoka Mwanza ambapo ni mbali 
zaidi.
Zipo frusa nyingi za uwekezaji 
hata kwenye soko la chakula cha kuku na wanyama wengine lakini kama wewe
 ni mwekezaji unaweza kufika huko ukajionea mwenyewe.
www.mobinday.blogsopot.com 0753399 579 mobinsons@yahoo.com 


No comments:
Post a Comment