Na Dotto Mwaibale
Watanzania  wametakiwa kudumisha  
na  kuithamini amani ya nchi iliyopo badala ya kuiharibu kwani 
kuirudisha kwake ikitoweka itachukua muda.
 Wito huo ulitolewa na Kiongozi wa
 Kanisa la Huduma ya Maombezi,  Nabii Flora Peter alipokuwa akihubiri 
katika ibada ya Krismasi katika Kanisa hilo lililoko Mbezi SalaSala Dar 
es salaam juzi.
“Kuwa na amani ni jambo jema kwa 
wananchi wote na dini zote lakini kuharibu amani ni jambo ambalo 
halimpendezi mungu” alisema Nabii Peter.
Alisema Tanzania inajivunia amani 
iliyopo ambayo imedumishwa na wanzania wenyewe hivyo kila mmoja 
mwananchi ana wajibu wa kuitunza.
Alisema mahli palipo kosekana amani hakuna jambo lolote linaloweza kufanyika ikiwa pamoja na kuabudu kwani mifano halisi inaonekana katika nchi zenye machafuko kama vile somaria, Siria na nyinginezo.
Alisema mahli palipo kosekana amani hakuna jambo lolote linaloweza kufanyika ikiwa pamoja na kuabudu kwani mifano halisi inaonekana katika nchi zenye machafuko kama vile somaria, Siria na nyinginezo.
“Katika nchi hizo watu wanahitaji 
kuabudu kama tulivyo sisi lakini wanashindwa kwa sababu hakuna amani 
hivyo tuidumishe amani tuliyo nayo” aliongeza Nabii Flora.
Alisema amani ya Tanzania 
idumishwe ili mataifa mengine yaje kujifunza kwetu kuliko kuiacha 
ikapotea kwa kugombana baina ya dini moja na nyingine.
 Alisema Tanzania imekuwa ni nchi 
ya mfano na gumzo kwa nchi nyingine kutokana na wananchi wake kuwa na 
upendo na utulivu wa kipee hata mtu akiwa nje ya nchi anakuwa kifua 
mbele kusema anatoka Tanzania hivyo ni jambo la kujivunia.
Katika hatua nyingine Nabii Peter amewataka waananchi wote bila kujali imani za dini zao kujitokeza kushiriki mchakato wa kujadili katiba mpya kwani ndiyo dira ya nchi yetu.
Katika hatua nyingine Nabii Peter amewataka waananchi wote bila kujali imani za dini zao kujitokeza kushiriki mchakato wa kujadili katiba mpya kwani ndiyo dira ya nchi yetu.
Alisema ni vizuri watu mbalimbali 
wakajadili kwa kina mchakatio wa katiba mpya badala ya kujadili chama 
kwani katiba ndiyo itakayaotuongoza kwani suala hilo ni letu sote na si 
la mtu au kundindi fulani.
Nabii Peter alitumia fursa hiyo kwa kumpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kukubali kupitisha mchakato wa katiba mpya pamoja na kuweka uhuru kwa kila mwananchi kufanya jambo lake kwa uhuru pasipo kuvunja sheria.
” Kila mtu anaona utawala wa Rais Kikwete jinsi unavyofanya kazi kwa uwazi na kasi kubwa na ndiyo maana kila idara na taasisi imepewa nafasi ya kuamua na mamuzi hayo yanaheshimiwa na kila mtu kwa maslahi ya Taifa” alisema Nabii huyo.

No comments:
Post a Comment