TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, December 25, 2012

WATEJA WAZIDI KUTAPELIWA NDANI YA CLUB ARBETO -MOSHI.

 Wakazi wa mji wa Moshi, wamezidi kulalamika kutokana na Tabia wanayofanyiwa na Waudumu wa Club na Bar ya CLUB ARBETO, ambapo Kamera yetu imefanikiwa kuwanasa wakiwa katika Mzozo mkali kati ya wateja ambao wanadai kutapeliwa fedha kwa kuongezewa Bill wakati wa Malipo.
Hali hiyo ambayo inazidi kuipolomosha zaidi Club hiyo inasadikiwa kwamba kuna baadhi ya watu ambao wanashiriki katika kuficha hali hiyo ambapo ujitokeza kuzuia wasipewe kipongo ama kuzalilishwa hao waudumu, hivyo uja watu na kujidai kwamba wao ni Maafisa wa Polisi na kuwataka kuachana na hao wanaodaiwa kutapeli kila kukicha.
hata hivyo pamoja na kutapeli Wateja pia lalamiko lingine kwa Club na Bar ya Arbeto ni pamoja na Huduma kuwa mbaya, inayotokana na Waudumu kutokuwa makini na pia Wateja kucheleweshewa Mahitaji pale wanapohitaji, hivyo mara nyingi wateja wanashindwa kusubiri na kuamua kuondoka.
"sijawahi kabisa kuona Waudumu wababaishaji kama hawa, Chakula nimeagiza yafika masaa mawili sasa, kwani wanadhani hapa mbinguni, maana hata njaa yenyewe imakatika na hata wakileta hicho chakula chao wale wenyewe, hata hamu ya kunywa bia pia imekata" alisikika mtu mmoja ambaye alijitambulisha kwa jina la mkurugenzi wa EGESHA TRADING
AIDHA wateja hao wamewataka kufanya haraka mabadiliko ya waudumu ili kuweza kuendana na historia nzuri ya Club hiyo tangu imejengwa" hapo zamani hapa ndiyo palikuwa sehemu yetu, lakini kama mwenye eneo asipofanya haraka kubadili waudumu na wafanyakazi, hatajikuta soko lote linakwenda katika eneo tofauti, na siku hizi hapa Moshi Hapatoshi kwa kumbi za starehe, angalia huduma ya pale Zumba Land, Club Malindi ama kule CLUB LA LIGA, mtu unapata huduma hadi unafurahi"alisema lauwo masawe
 Baada ya Kasheshe kutimuka ndani ya Arbeto Club, jamaa anayeongea na Simu, alijitambulisha kama Afisa wa Polisi na Kufanya Jaribio la kukataza Mwandishi wa Habari hizi asifanye kazi yake lakini hata hivyo Mwandishi huyo ambaye amepewa ulinzi mkubwa wa mabaunsa,ikiwa ni pamoja na huyo mlinzi na anayeonyesha kidole. mwenye kijani ni afisa wa intergreted ambaye alikuwa akifanya uchunguzi kuhusu tukio hilo.
 Watu ambao wanatumia Gari lenye namba za Usajili T-829-AFZ, ambao walijitambulisha kama Maafisa wa Polisi katika kuzuia Waudumu wasipewe adhabu ama kupelekwa Sehemu husika kwa uchunguzi., hapa wakiwa wameshindwa kuzuia Kamera na Mwandishi asifanye kazi yake baada ya kuzibitiwa na Walinzi wa Huyo Mwandishi.
 Wahudumu wakiwa katika hali ya Mshituko mara baada ya Dili lao la kutapeli Wateja kwa kuwaongezea Bill kusanuka.
 Baadhi ya Meza za wateja wakiwa katika Malalamiko Makali juu ya Huduma za Club hiyo ya Arbeto kuwa mbaya.
 Waudumu wakiwa wamejikunyata baada ya kupewa Vijembe na Meza za Wateja ambao tayari walikuwa wamefanyiwa matendo hayo.(kulia ni Mwandishi wa Gazeti la KIU, ndugu Mwinyi ambaye pia alikuwa kama shuhuda wa Tukio hilo.
 Hali ikiwa si shwari kutoka ndani ya Arbeto Club, Wateja wakiwa wanaondoka eneo hilo, huku watu walijitambulisha kama Maafisa wa Polisi wakiwa ndiyo wanaingia mara baada ya kupigiwa simu na Hao wafanyakazi wa eneo hilo.
 Ndani ya Arbeto kukiwa kumechafuka
 hali ikiwa si shwari na kusababisha wateja kutoingia ndani
 Watu ambao walijitambulisha kama maafisa wa Polisi wakiwa wanatafakari jinsi ya kufanya kuzuia kutozalilishwa kwa Wafanyakazi hao.
 Baadhi ya Wakazi wa Moshi wakiwa Pembezoni mwa Eneo hilo huku wakitafakari(Picha Zote na Mwandishi Wetu kutoka MOSHI.

No comments:

Post a Comment