Waziri
 wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara  (kulia) 
akimsikiliza Mwenyekiti wa kikundi cha Nyakalalo kililopo  kijiji cha 
Kitigiri wilayani Geita, Gideon Msabila (kushoto)  ambaye alimuelezea 
jinsi walivyonufaidika na mkopo wa mfuko wa maendeleo ya vijana fedha 
ambazo zimewawezesha kufungua duka  la rejareja la bidhaa za nyumbani. 
  Picha na Anna Nkinda – Maelezo
Waziri
 wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara  (kulia) 
akimsikiliza Mwenyekiti wa kikundi cha Bodaboda kilichopo kijiji cha 
 Bugalama  wilayani Geita,  Enos Komanya  wakati alipotembelea kikundi 
hicho ambacho kilipata mkopo  kutoka mfuko wa maendeleo wa halmashauri. 
Waziri Dk. Mukangara  alitembelea kijiji hicho jana ili kuona fedha za 
mkopo zilizotolewa na mfuko wa maendeleo ya vijana zimewasaidiaje vijana
 kujikwamua kimaisha.
Vijana
 wa kikundi cha kusaidiana kulima cha Busaka katika kijiji cha Kitigiri 
wakifurahia fedha shilingi 50,000/= walizopewa jana na Waziri wa Habari,
 Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara  (wanne kulia) kwa 
ajili ya kununulia soda za sikukuu ya Krismasi . Waziri Dk. Mukangara 
 aliwahimiza vijana hao kujiunga kwenye vikundi vya maendeleo vya kilimo
 ili weweze kupata mkopo wa kununulia pembejeo na kuweza  kuzalisha 
chakula kwa wingi zaidi.
Waziri
 wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara  (wanne 
kulia) akiwa katika picha ya pamoja  na viongozi wa wilaya ya Geita, 
Kata ya Bukondo na  kijiji cha Kitigiri mara baada ya kumaliza ziara 
yake katika kijiji  hicho jana ili kuona fedha za mkopo za mfuko wa 
maendeleo ya vijana  zimewasaidiaje vijana kujikwamua kiuchumi. 
……………………………………………………
Na Anna Nkinda – Maelezo, Geita
 Vijana  wametakiwa kushiriki 
katika suala la ulinzi na usalama wa maeneo wanayoishi kwa kujiunga na 
vikundi vya ulinzi shirikishi ili kulinda na kusimamia rasilimali za 
vijiji vyao.
Hilo litafanikiwa endapo vijana 
 watakuwa na moyo wa kujituma  na kutambua kuwa wanajukumu la kujenga 
taifa kwa kuhakikisha kuwa wanajiletea maendeleo yao na nchi kwa ujumla 
kutokana na  kazi mbalimbali wanazozifanya.
Rai hiyo imetolewa  mjini hapa 
jana  na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella 
Mukangara  wakati akiongea kwa nyakati tofauti na wanavikijiji vya 
Bugalama na Kitigiri vilivyopo wilayani Geita alipozitembelea baadhi ya 
Vyama vya Kuweka Akiba na Kukopa (SACCOS) zilizopata mkopo  kupitia 
mfuko wa maendeleo wa vijana na fedha za maendeleo ya mfuko wa 
Halmashauri.
Dk. Mukangara alisema kuwa 
maendeleo ya nchi yanawategemea vijana ambao ndiyo nguzo ya taifa  hivyo
 basi wizara yake kupitia halmashauri za wilaya itahakikisha kuwa inatoa
 mafunzo ya kuwajengea uwezo vijana jambo la muhimu ni kujiunga katika 
vikundi vya maendeleo ili waweze kufikiwa kwa urahisi.  
“Uongozi wa kijiji uhakikishe kuwa
  unawahimiza  vijana na kuwajengea  uwezo katika mtazamo wa 
kujitengemea, kujituma na kufanya kazi na  kujiunga kwenye vikundi vya 
maendeleo  ili iwe rahisi kupata mkopo kupitia SACCOS zilizopo vijijini 
mwenu” alisema Dk. Mukangara.
Aliwataka wanakijiji hao 
 kuwasimamia vijana wao ili wanawajibike na  kutambua  kuwa wanajukumu 
kubwa la kuhakikisha kuwa wanashiriki katika shughuli za kilimo cha 
chakula na biashara jambo ambalo litasababisha kuwa na chakula cha 
kutosha na kuepukana na janga la njaa.




No comments:
Post a Comment