TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, December 27, 2012

Waziri Dk. Mukangara alipotembelea ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kagera

 
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara  (kulia) akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera  Kanali Mstaafu Fabian Massawe mara baada ya kumtembelea ofisini kwake leo mjini Bukoba. Waziri Dk. Mukangara yupo mkoani humo kwa ajili ya kuangalia jinsi  fedha za mkopo kutoka mfuko wa vijana  zilivyoweza kuwasaidia vijana kujikwamua kimaisha.
 
Mkuu wa Mkoa wa Kagera  Kanali Mstaafu Fabian Massawe (kushoto) akimsomea taarifa fupi ya mkoa wake Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara  (kulia ) alipomtembelea ofisini kwake leo mjini Bukoba. Waziri Dk. Mukangara yuko mkoani Kagera  kwa ajili ya kuangalia jinsi  fedha za mkopo kutoka mfuko wa Maendeleoa ya vijana   zilivyoweza kuwasaidia vijana kujikwamua kiuchumi.
 
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara  (kushoto) akimsikiliza  Mkuu wa Mkoa wa Kagera  Kanali Mstaafu Fabian Massawe alipomtembelea ofisini kwake leo mjini Bukoba. Waziri Dk. Mukangara yupo mkoani humo kwa ajili ya kuangalia jinsi  fedha za mkopo kutoka mfuko wa vijana  zilivyoweza kuwasaidia vijana kujikwamua kimaisha.
 
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara  (kushoto ) akiongea na viongozi wa mkoa wa Kagera (hawapo pichani) leo mjini Bukoba jinsi  Serikali inavyoangalia uwezekano wa kuongea mkopo kwa SACCOS zinazolenga shughuli za maendeleo ya vijana  kutoka shilingi milioni tano hadi kumi kutokana na mahitaji ya fedha hizo kuwa makubwa. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana James Kajugusi.
 
Baadhi ya viongozi wa mkoa wa Kagera wakimsikiliza  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara  (hayupo pichani) wakati akiongea nao kuhusu umuhimu wa kuwafuatilia vijana kwa ukaribu katika Kata na kuweza kuwafundisha na kuwashirikisha  katika miradi ya maendeleo
  Picha na Anna Nkinda – Maelezo

No comments:

Post a Comment